in

Nokia Kurudi na Toleo Jipya la Simu ya Nokia X6 (2018)

Nokia X6 (2018) itakuwa simu ya kwanza ya Nokia kuwa na Notch

Nokia X6 2018 mpya

Kampuni ya Nokia inajiandaa kurudi na toleo jipya la simu mpya ya Nokia X6 (2018) ambayo inategemewa kuzinduliwa siku ya ijumaa mwezi huu. Hapo awali Nokia X6 ilishwahi kuwa simu ya zamani kutoka Nokia ambayo ilikuwa ikitumia mfumo wa uendeshaji wa Symbian kabla ya kampuni hiyo kujiunga rasmi na mfumo wa Android.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, simu hiyo itazinduliwa rasmi siku hiyo ya ijumaa huko nchini china na itakuwa simu ya kwanza kabisa kwa kampuni ya Nokia kuwa na ukingo wa juu maarufu kama Notch.

Mbali na hayo simu hiyo pia inategemewa kuja na kamera mbili kwa nyuma pamoja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo itakuwa kwa nyuma kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu. Simu hii pia itakuja na kioo cha touchscreen chenye ukubwa wa inch 5.8 pamoja na aspect ratio ya 19:9. Vilevile simu hii ya Nokia X6 (2018) itakuja processor ya MediaTek Helio P60 chipset, ambayo itakuwa ikisaidiwa na RAM ya 4GB pamoja na mfumo wa uendeshaji wa Android Oreo.

Inasemekana pia simu hii itakuja na matoleo mawaili, toleo moja likiwa na uwezo wa RAM ya GB 4 na toleo lingine litakuja na uwezo wa RAM ya GB 6 huku ikiendeshwa na processor ya Snapdragon 636. Simu hizo zote za Nokia X6 (2018) zinatarajiwa kuzinduliwa nchini china na zitauzwa kuanzia Yuan ya China 1,799 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 650,000.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Endelea kutembelea Tanzania Tech, tutakujuza sifa kamili za simu hii pindi itakapo zinduliwa rasmi hapo tarehe 27 mwezi huu.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.