Samsung-Galaxy-S8 Mpya

Hii Ndio Picha Iliyovuja ya Simu Mpya ya Samsung Galaxy S8

Picha za tetesi za simu mpya ya Samsung Galaxy S8 zimekua nyingi sana, ukitegemea simu hiyo inatarajiwa kutoka mwezi February basi tetesi nazo zimezidi kuwa nyingi sana. Lakini leo uko nchini china kupitia tovuti ya Weibo service zimevuja picha ambazo zinasemekana ndio picha halisi za simu hiyo mpya kutoka kampuni ya Samsung.

Hii Ndio Picha Iliyovuja ya Simu Mpya ya Samsung Galaxy S8 1
Picha kutoka Weibo

Picha hii inasemekana ndio picha halisi ya simu mpya ya Samsung Galaxy S8 lakini bado hakuna uhakika kama simu hiyo ndivyo itakavyokuwa, lakini kwa mtazamo tu uwezekano wa simu hii kuwa ndio samsung galaxy s8 ni mkubwa sana.

Ngoja tuone kwenye uzinduzi wa simu hiyo utakaofanyika mapema mwezi February kwenye mkutano wa CES wa Mwaka 2017, Kujua zaidi kuhusu simu hii na kuangalia uzinduzi wa simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech pamoja na kipengele cha CES 2017 kila siku.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
MKUTANO CES 2017
Matukio Yote Yaliyojiri Jana Kwenye Mkutano wa CES 2017
Next Post
teknolojia bora CES 2017

Bidhaa Bora Mpaka Sasa Kwenye Mkutano wa CES 2017