Mfuniko wa Kamera

Hichi ni Kifaa Kipya cha Kufunika Kamera ili Kuzuia Wadukuzi

Kuna stori mbalimbali duniani ambazo zina elezea matukio ya wadukuzi kutumia kamera ya mbele ya kifaa chako kukupeleleza na baadae kutuma video hizo mtandaoni. Wote tunajisikia huru mbele ya vifaa vyetu, ukijiuliza tu ni mambo mangapi umefanya mbele ya simu au kompyuta yako kwa kweli ni mengi sana, sasa jiulize maisha yako yote mbele ya kifaa chako yakitumwa kwenye internet itakuaje..?

Kusuluhisha hilo kampuni moja ya nchini marekani imetengeneza kava maalum kwaajili ya kuziba kamera yako. Kifaa hicho kilichopewa jina la IS|CC ni kikava kidogo sana chenye uwezo wa kufunika kamera ya simu, kompyuta au hata web cam ili kukupa uhuru zaidi mbele ya kifaa chako.

https://www.youtube.com/watch?v=no41wf_BKmQ

Intelligent Security | Camera Cover kwa sasa kipo kwenye hatua za mwisho za utengenezaji na kitapatikana hivi karibuni kwenye masoko mbalimbali za mtandaoni.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play store, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza kwa njia ya video.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Laptop Bora Kwaajili ya Kucheza Game Mwaka Huu (2018) 1
Laptop Bora Kwaajili ya Kucheza Game Mwaka Huu (2018)
Next Post
facebook storiesz

Facebook Nayo Kuleta Sehemu Mpya ya Facebook Stories