in

Jinsi ya Kupata Namba ya Simu ya Nje ya Nchi Bure

Tumia njia hii kuweza kupata namba yako ya simu ya nje ya nchi

Jinsi ya Kupata Namba ya Simu ya Nje ya Nchi Bure

Inawezekana kwa namna yoyote ukawa na uhitaji wa kupigiwa simu na watu kutoka nje ya nchi na uhitaji kutumia mitandao kama WhatsApp na mitandao mingine.

Kupitia maujanja haya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kupata namba yako ya simu ya nje ya nchi na unaweza kutumia kupiga na kupigiwa simu bure kabisa, pia unaweza kutumia namba hiyo kusajili mitandao ya kijamii kama WhatsApp na mitandao mingine.

Kwa kuanza unahitaji vitu kadhaa, kitu cha kwanza cha muhimu ni Internet, unahitaji angalau kiasi cha MB 200 na kuendelea, pia unatakiwa kuwa na akaunti ya Facebook au Google. Kama tayari unavyo vitu vyote hivi basi unaweza kuendelea hatua inayofuata.

Hatua ya kwanza Download app hapo chini kisha install kwenye simu yako, kwa sasa app hii haipo kwa Tanzania hivyo hakikisha unapakua app hii kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii, subiri kwanza na Husijisajili kupitia app hiyo, unacho takiwa kufanya moja kwa moja bofya hapo chini na utapelekwa kwenye tovuti rasmi ya App hiyo, kisha tengeneza akaunti yako kwa kutumia akaunti yako ya Google, baada ya hapo sasa unaweza ku-login kwa kutumia akaunti yako yako kupitia app uliyo download moja kwa moja.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Tembela Tovuti Hapa

Baada ya hapo unaweza kuangalia video hapo chini kujua jinsi ya kutumia app hii na kupata namba yako ya simu ya nje ya nchi moja kwa moja kupitia simu yako ya Android.

Njia hii itakusaidia sana kupiga simu za nje ya nchi na pia utaweza kupata namba ya simu ambayo utaweza kutumia kupiga simu kwa urahisi na haraka, pia unaweza kupigiwa ndani ya namba yako moja kwa moja.

Kitu cha msingi hakikisha namba yako unaitumia kwani usipo itumia kwa muda mrefu namba hiyo inaweza kufutwa na kupewa mtu mwingine au inaweza kufutwa kabisa na hutoweza kuipata.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujia jinsi ya kuona namba ya simu ya mtu yoyote ambaye unachati nae kwenye mtandao wa Facebook.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

15 Comments