in

Badilisha Simu Yako Kuwa Kama iPhone 12 (Pakua Wallpaper)

Download Hapa wallpaper Halisi za iPhone 12

Badilisha Simu Yako Kuwa Kama iPhone 12 (Pakua Wallpaper)

Kama wewe ni mpenzi wa simu ya iPhone 12 na kwa muda ulikuwa unataka simu yako ionekane kama iphone 12 basi unasoma makala sahihi. Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ya kubadilisha simu yako kuwa na muonekano kama wa iPhone 12.

Kwa siku ya leo tuta angalia zaidi kwenye muonekano wa juu ambapo unaweza kupakua wallpaper halisi au Original za iPhone 12, ikiwa pamoja na app ambayo itaweza kusaidia kubadilisha icon za simu yako kwa urahisi.

Kupitia hapo chini utaweza kupakua wallpaper halisi za iPhone 12 na iPhone 12 Pro, kama ulikuwa unahitaji wallpaper hizo unaweza kupakua hapo chini.

Download iPhone 12 Wallpaper HD

Baada ya kupakua Wallpaper hizo, moja kwa moja hifadhi kwenye simu yako kisha pakua app hapo chini alafu install vizuri kwenye simu yako. Baada ya kuinstall fungua na moja kwa moja utapata muonekano wa mfumo wa iOS 14.

Download App Hapa

Baada ya hapo sasa weka wallpaper ambazo umepakua awali kupitia link hapo juu, moja kwa moja utakuwa umepata muonekano wa iPhone 12 moja kwa moja kwenye simu yako ya Android.

Menu za Siri Ambazo Ulikuwa Huzijui Kwenye Windows 11

Mpaka hapo natumani utakuwa umweza kubadilisha simu yako ya Android kuwa na muonekano wa kama wa iPhone 12, kama unataka kubadilisha simu yako kuwa kama Galaxy S21 basi unaweza kusoma makala iliyopita hapa. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.