Badilisha Muonekano wa Simu Yako Kuwa kama Galaxy S21

Fanya simu yako iwe na muonekano kama simu mpya za Galaxy S21
Badilisha Muonekano wa Simu Yako Kuwa kama Galaxy S21 Badilisha Muonekano wa Simu Yako Kuwa kama Galaxy S21

Hivi karibuni kampuni ya Samsung imezindua simu mpya za Galaxy S21, simu hii ni moja kati ya simu bora za Samsung ambazo unaweza kununua kwa sasa.

Japo kuwa bei ya Galaxy S21 kwa kipindi hichi ipo chini kidogo, lakini pengine kwa sasa bado hujafikiria kubadilisha simu yako. Kuliona hilo hivi leo nimekuletea wallpaper halisi za Samsung Galaxy S21, ambazo unaweza kuweka kwenye simu yako na kubadilisha muonekano wa simu yako ili ufanane angalau kidogo na muonekano wa simu hizo mpya.

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa simu za Samsung, basi ni wazi utakuwa unajua kuwa Samsung hutengeneza wallpaper ambazo huendana na vioo vya simu zake hasa vioo vya Super AMOLED.

Advertisement

Hivyo basi kama unayo simu yenye kioo cha Super AMOLED ni wazi utaweza kufurahia sana wallpaper hizi, ikiwa pamoja na kutunza chaji zaidi kwenye simu yako kwa kuwa wallpaper hizi zimetengenezwa maalum kwaajili ya kufanya hivyo.

Mbali ya kupata wallpaper original za Galaxy S21, pia utaweza kuata live wallpaper ambazo unaweza kuweka kwenye sehemu ya muito kama unataumia simu ya Samsung yenye mfumo mpya wa Android 11 na One UI 3.0. Unaweza kudownload Wallpaper na Live Wallpaper kupitia link hapo chini.

Download Wallpaper Hapa

Kama unataka wallpaper za live ambazo zipo kwenye mfumo wa mp4 unaweza kudownload kupitia link hapo chini.

Download Live Wallpaper Hapa

Wallpaper hizi ni Original kabisa kutoka kwenye simu zote za Samsung Galaxy S21 na zinakuja na resolution bora inayoweza kukaa kwenye simu yoyote hata yenye uwezo wa 4K. Kama wewe ni mpenzi wa wallpaper basi unaweza kupakua wallpaper za iPhone Hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use