Soma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online (Njia Bora)

Sasa soma meseji unazotumiwa kwa siri bila mtu yoyote kujua
Soma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online (Njia Bora) Soma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online (Njia Bora)

Ni wazi kuwa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza kukufanya uwe na uhitaji wa kusoma meseji uliyotumiwa kupitia programu ya WhatsApp bila programu hiyo kuonyesha kama upo “online” au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia ili kujibu meseji zako za WhatsApp unazotumiwa bila programu ya WhatsApp kuonyesha kama upo online au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo yaani tiki mbili za blue.

Najua kila mtu anaweza kusema najua hiyo lakini nakushauri endelea kusoma makala hii hadi mwisho kwani unaweza kupata maujanja mapya ambayo pengine ulikuwa hujui kwa namna moja ama nyingine. Kama kawaida sipendi kupoteza muda wako mwingi kwa maneno yangu, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia ya kwanza.

Advertisement

Njia ya Kwanza

Najua kuwa unaweza kusema kuwa unaweza kuondoa last seen kwenye programu yako ya WhatsApp ili mtu asiweze kujua kama umesoma meseji zake, lakini je vp na wewe ukitaka kuona meseji ulizo mtumia mtu kama zimefika..?

Kuliona hili leo nimekuletea njia nyingine rahisi sana ambayo mtu hatoweza kuona kama umesoma meseji hata kama sehemu ya last seen imewashwa.

Unacho takiwa kufanya ni kusoma meseji za WhatsApp kupitia sehemu ya Notification. Sehemu hii inapatikana juu kabisa kwenye simu yako na hapo ndipo jumbe zote zinapo pitia kabla ya kuonekana ndani ya programu husika.

Unachotakiwa kufanya ni kuvuta sehemu hiyo ya juu pale unapo pata ujumbe kisha bofya sehemu ya reply na kisha jibu ujumbe huo ulio tumiwa. Kwa kufanya hivyo meseji itajibiwa bila kuonyesha kama upo online au kama umesoma meseji hiyo. Hivyo haita onyesha kama umesoma meseji husika.

Soma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online (Njia Bora)

Njia ya Pili

Njia ya pili unahitaji kupakua programu ya programu app chini, hii itakusaidia kusoma meseji za WhatsApp, Instagram, Telegram na mitandao mingine mingi bila kuonekana “online”. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kusoma meseji za WhatsApp bila kuonekana basi njia hii ni njia bora zaidi.

Mbali na kuonekana online app hii pia inasaidia kuzuia tiki mbili za blue ambazo huonyesha kuwa meseji imesomwa.

Unaweza kupata app hii kupitia link hapo chini na hakikisha kuwa una install na kutoa ruhusa zote kwenye app hiyo na moja kwa moja uta anza kusoma meseji za WhatsApp unazotumiwa bila mtu kujua kama umesoma meseji hizo.

Download App Hapa

Kama unataka kujua zaidi kuhusu app hii unaweza kuangalia video hapo juu. Lakini kama unataka kuwasha muonekano wa giza kwenye programu yako ya WhatsApp unaweza kusoma hapa. Pia hivi unajua kuwa unaweza kutengeneza pesa kupitia WhatsApp.? Kama ulikuwa hujui basi soma hapa kuanza kutengeneza pesa sasa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use