in

Apple Yazindua iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020)

Hizi hapa sifa pamoja na bei ya iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020)

Apple Yazindua iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020)

Kampuni ya Apple hivi leo imetangaza kuzindua matoleo mapya ya iPad Pro 12.9 (2020) pamoja na iPad Pro 11 (2020). Matoleo haya ni matoleo ya maboresho ya iPad Pro 12.9 ya mwaka (2018) pamoja na iPad Pro 11 ya mwaka (2018).

Hata hivyo iPad Pro zote zilizo zinduliwa siku ya leo zinakuja na maboresho makubwa kwenye upande wa kamera, processor pamoja na programu mpya za AR kutoka Apple.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Apple Yazindua iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020)

Tukianza na upande huo wa kamera, iPad Pro 11 na iPad Pro 12.9 (2020) inakua na kamera mbili kwa nyuma, kamera kuu ikiwa na Megapixel 12 na kamera nyingine ikiwa inakuja na Megapixel 10 ambayo ni ultrawide. Kamera zote mbili kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K 60fps, huku zikiwa na Flash ya Quad-LED dual-tone flash na TOF 3D LiDAR scanner.

Apple Yazindua iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020)

Kwa upande wa mbele, iPad Pro (2020) zinakuja na kamera ya selfie ya Megapixel 7 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30/60fps. Kamera hizo pia zinakuja na uwezo wa Face detection, HDR, pamoja na panorama.

Kwa upande wa processor iPad hizi mpya zinakuja na processor ya Apple A12Z Bionic, ambayo inasemekana kuja na maboresho makubwa huku ikiwa na eight-core CPU pamoja eight-core GPU pamoja na aina mpya ya mfumo wa kupooza processor hiyo. Mbali na processor iPad hizi zote zinakuja na uhifadhi wa ndani wa kuchagua kati ya GB 128, GB 256, GB 512 pamoja na Terabyte 1.

Mabadiliko mengine kwenye iPad Pro hizi mpya ni pamoja na aina mpya ya keyboard ambayo inawezesha iPad hizi mpya kutumika kama kompyuta. Unaweza kutumia pia sehemu mpya ya trackpad ambayo inaweza kusaidia kutumia iPad Pro (2020) bila kugusa kioo. Keyboard hiyo inaweza ku-unganishwa kwa kutumia waya wa USB au Bluetooth. Sifa nyingine za iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020) ni kama zifuatazo.

Sifa za Apple iPad Pro 11 (2020)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 11.00 chenye teknolojia ya LED-backlit IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1668 x 2388 pixels, na uwiano wa (~265 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iPadOS 14.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4x Vortex + 4x Tempest).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12Z Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (7-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko iPad za aina nne iPad moja inakuja na GB 128, GB 256 nyingine GB 512 pamoja na nyingine inakuja na TB 1 zote zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
  • Ukubwa wa RAM – Bado haijajulikana
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa Face detection, HDR na panorama.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Zipo kamera mbili, moja inakuja na Megapixel 12 yenye f/1.8, 1/3″, PDAF, na nyingine inakuja na Megapixel 10 yenye f/2.4, 11mm (ultrawide) huku zikiwa zina HDR, pamoja na Quad-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po battery (28.65 Wh) yenye teknolojia ya kuweza kuchaji simu nyingine pamoja na Fast charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Silver na Space Gray
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Nano-SIM / Electronic SIM card (Apple e-SIM), haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, barometer
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi wa Face ID.

Sifa za Apple iPad Pro 12.9 (2020)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 12.9 chenye teknolojia ya LED-backlit IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 2048 x 2732 pixels, na uwiano wa (~265 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iPadOS 14.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4x Vortex + 4x Tempest).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12Z Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (7-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko iPad za aina nne iPad moja inakuja na GB 128, GB 256 nyingine GB 512 pamoja na nyingine inakuja na TB 1 zote zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
  • Ukubwa wa RAM – Bado haijajulikana
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa Face detection, HDR na panorama.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Zipo kamera mbili, moja inakuja na Megapixel 12 yenye f/1.8, 1/3″, PDAF, na nyingine inakuja na Megapixel 10 yenye f/2.4, 11mm (ultrawide) huku zikiwa zina HDR, pamoja na Quad-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po battery (36.71 Wh) yenye teknolojia ya kuweza kuchaji simu nyingine pamoja na Fast charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Silver na Space Gray
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Nano-SIM / Electronic SIM card (Apple e-SIM), haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, barometer
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi wa Face ID.

Bei ya iPad Pro 12.9 (2020) na iPad Pro 11 (2020)

Kwa mujibu wa Apple, iPad Pro (2020) zote zinapatikana kwa bei ya zamani ambapo, bei ya iPad Pro 12.9 (2020), yenyewe itaanzia dollar za marekani $1000 ambayo ni sawa na Tsh 2,300,000 hadi dollar za marekani $1,150 ambayo ni sawa na Tsh 2,650,000 kwa iPad Pro 12.9 (2020) yenye LTE pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128.

Kwa upande wa bei ya iPad Pro 11 (2020), itauzwa kuanzia dollar za marekani $800 ambayo ni sawa na Tsh 1,844,000 kwa toleo linalotumia WiFi na dollar $950 ambayo ni sawa na Tsh 2,190,000 kwa iPad Pro ya inch 11 yenye kutumia LTE. Kumbuka bei hizi inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Bei ya iPad Pro-Magic Keyboard

Apple Yazindua iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020)

Kwa upande wa bei ya keyboard ya iPad Pro inayojulikana kama iPad Pro-Magic Keyboard, itauzwa kwa dollar za marekani $299 sawa na takribani TZS 670,000 bila kodi kwa iPad Pro ya inch 11, na iPad Pro ya inch 12.9 Magic Keyboard yake itauzwa kwa dollar za marekani $349 sawa na takribani TZS 805,000 bila kodi. Bei hizi zinaweza kubadilika kwa Tanzania.

Apple Yazindua iPad Pro 11 (2020) na iPad Pro 12.9 (2020)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.