in

Programu za Kusaidia Kudownload Kwa Haraka (Windows)

Hizi hapa programu mbadala wa programu ya IDM ya Windows

Programu za Kusaidia Kudownload Kwa Haraka (Windows)
Online download

Najua kuwa nikisema programu za kudownload kwa haraka kwenye kompyuta hasa za Windows wote mawazo yenu yanaweza kuwa kwenye programu ya IDM au Internet Download Manager. Japo kuwa programu hii ni bora na ina uwezo mkubwa wa kusaidia kudownload kwa haraka, lakini leo kwenye makala hii tutaenda kuongelea programu nyingine ambazo zinaweza kuwa bora kwa namna moja ama nyingine kwenye kompyuta yako ya Windows.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta mbadala wa programu ya IDM basi makala hii itakusaidia sana, basi bila kupoteza muda twende tukangalie programu hizi.

Free Download Manager

Programu za Kusaidia Kudownload Kwa Haraka (Windows)

Free Download Manager ni moja kati ya programu bora sana za kudownload kwenye kompyuta, programu hii ni nzuri kwa sababu inakuja na mfumo kama wa IDM ambapo unaweza kudownload file kwa haraka kama IDM inavyofanya. Tofauti na IDM programu hii yenyewe ni bure kabisa kuitumia na utapata kila kia kitu ambacho programu ya IDM inafanya.

Download Free Download Manager

JDownloader 2

Programu za Kusaidia Kudownload Kwa Haraka (Windows)

JDownloader 2 ni programu nyingine bora ambayo itakusaidia kudowload kwa haraka kwenye kompyuta yako, uzuri wa programu hii ni kuwa unaweza kupakua mafile mengi kwa wakati mmoja ikiwa pamoja na uwezo wa kupakua video kutoka kwenye tovuti maarufu duniani. Mbali ya hayo, kupitia JDownloader 2, utaweza kuongeza uwezo wa programu hii kwa kutumia plugins ambazo zinapatikana kupitia tovuti ya programu hii.

Download JDownloader 2

Ninja Download Manager

Programu za Kusaidia Kudownload Kwa Haraka (Windows)

Ninja Download Manager ni programu nyingine ambayo itakusaidia kudownload kitu chochote kwenye kompyuta yako kwa haraka, programu hii ni bora na inakuja na muonekano mzuri pengine kuliko programu nyingine kwenye list hii. Uzuri wa programu hii ni kuwa una uwezo wa kupakua file kwa muda maalum, yaani kwa mfano una uwezo wa kuset file liweze kudownload kuanzia saa mbili usiku au muda wowote ambapo utakuwa unahitaji.

Download Ninja Download Manager

EagleGet

Programu za Kusaidia Kudownload Kwa Haraka (Windows)

EagleGet ni programu nyingine ambayo inakusaidia sana kudownload kwa haraka kwenye kompyuta yako, uzuri wa programu hii ni kuwa inakuja na uwezo maalum wa kuangalia mafile yote unayo pakua kama yanakuja na virus au malware. Tofauti ya programu hii na nyingine kwenye list hii ni kuwa, programu hii inakuja na vifurushi vya kununua lakini unaweza kupakua bure huku programu hiyo ikiwa na matangazo mbalimbali.

Download EagleGet

uGet

Programu za Kusaidia Kudownload Kwa Haraka (Windows)

UGet ni programu nyingine ambayo itakusaidia sana kupakua mafile yote kwa haraka, programu hii nayo inakuja na uwezo kama wa IDM na utaweza kupakua mafile kwa haraka bila kuangaika. Programu hii pia ina uwezo wa kupakua mafile mengi sana kwa wakati mmoja na inauwezo wa kupakua mafaili yote kwa haraka.

Download uGet

Na hizo ndio baadhi ya programu ambazo zinaweza kukusaidia kudownload mafile kwa haraka kupitia kompyuta yako ya Windows, kumbuka baadhi ya programu kwenye list hii zinaweza kufanyakazi kwenye mfumo wa macOS pamoja na Linux, kama unatumia mifumo hiyo basi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kwani tutakuletea makala inayohusu programu za kudownload haraka kupitia mifumo hiyo.

Kwa habari zaidi za teknolojia na makala kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa YouTube, ili uweze kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo.

Apps Nzuri za Kujaribu Kwenye Simu Yako ya Android (2021)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments