in

Habari Kubwa za Teknolojia Wiki ya #1 Mwezi wa Nane (2018)

Hizi hapa ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii

habari kubwa za teknolojia wiki hii

Kama wewe ni msomaji na mfuatiliaji wa maswala ya teknolojia basi inawezekana ulipitwa na habari mbalimbali za teknolojia kwa wiki hii inayoisha, hivyo kupitia kipengele hichi cha Tech Wiki tunakutea mfululizo wa habari kubwa za teknolojia kwa wiki nzima ikiwa pamoja na link ambazo zitakusaidi kwenda kusoma makala husika.

Najua kipengele hichi hakikwepo kwa muda lakini sasa kimerudi na tutakuwa tukiendelea kukuletea habari zote kubwa za teknolojia kila wiki ili kukusaidia kuweza kusoma habari zote za teknolojia kama ulikuwa bize kwa wiki nzima. Basi bila kupoteza muda twende tukanagalie habari kubwa kwa wiki hii inayoishia leo tarehe 12-08-2018.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kampuni ya LG wiki hii ilizindua simu yake mpya ya LG Q8, Simu ambayo ni tofauti kabisa na simu ya mwaka jana 2017 ambayo nayo pia ilikuwa na jina la LG Q8. Simu hiyo inakuja na Sifa nzuri na inakuja na ikiwa inauzwa takribani Tsh 1,095,000 bila kodi.

Kampuni ya Google ambayo ndio watengezaji wa mfumo wa Android, wiki hii imatangaza rasmi kuwa sasa iko tayari kutoa mfumo mpya wa Android 9 Pie. Kabla ya hapo mfumo wa Android 8 Oreo ndio ulikuwa mfumo mpya ambao hadi sasa bado haujawafikia watumiaji wengi wa simu za Android.

Wiki hii tulipata nafasi ya kuweza kuona muonekano wa simu mpya za iPhone, muonekano huu ndio muonekano halisi wa simu mpya za iPhone ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao. Simu hizo ambazo bado majina yake hayana uhakika ni pamoja na iPhone X mpya, iPhone X Plus, na iPhone Lite.

Wiki hii pia tulipata makala kutoka tovuti ya mwananchi iliyokuwa ikitoa ufafanuzi kidogo kuhusu baadhi ya vingamuzi kuacha kuonyesha chaneli za ndani au (local channels).

Wiki hii habari kubwa ilikuwa ni kuhusu uzinduzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9, Uzinduzi huu ulifanyika huko nchini marekani na uliuthuriwa na waandishi mbalimbali wa habari za teknolojia. Tanzania Tech tulifanikiwa kuonyesha uzinduzi huo mubashara kabisa kupitia tovuti yetu.

Baada ya kuangalia uzinduzi wa Galaxy Note 9 tulipaa nafasi ya kuweza kujua sifa zake na kama kawaida tuliweza kuonyesha sifa zake kamili pamoja na muonekano wa simu hiyo mpya ambayo inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia tarehe 24 mwezi huu wa nane.

Kama ukufanikiwa kuangalia mkutano wa uzinduzi wa Galaxy Note 9 usiwe na wasiwasi, wiki hii tulipata nafasi ya kuweza kukujuza yote ya muhimu yaliyotangazwa kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa simu hiyo pamoja na kuongele hata baadhi ya maboresho ya simu hiyo mpya.

Na hizo ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii ya kwanza ya mwezi wa nane, kwa habari zaidi hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku au ili kupata habari mpya pindi zinapotoka unaweza kupakua app ya Tanzania Tech kupitia mifumo yote ya Android pamoja na iOS. Hadi wiki ijayo nakutakia Jumapili njema na Mungu akubariki sana..!.

Habari Kubwa za Teknolojia Wiki ya #1 Mwezi wa Nane (2018)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments