in

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Simu Mpya ya LG Q8 (2018)

Fahamu sifa na bei ya simu mpya kutoka LG

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Simu Mpya ya LG Q8 (2018)

Kampuni ya LG katikati ya mwezi wa Tano mwaka huu 2018 ilizindua simu mpya ya LG Q7, hivi karibuni kampuni hiyo imerudi tena na toleo jipya la LG Q8 (2018), Simu hii mpya inakuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na kioo kikubwa pamoja na muonekano bora zaidi.

Simu hii ya LG Q8 (2018) inakuja na kioo cha inch 6.2 chenye teknolojia ya Full Vision IPS LCD display chenye resolution ya 1080 x 2160 pixels pamoja na aspect ratio ya 18:9 ratio. Simu pia hii inakuja na  processor ya Snapdragon 450 Octa core CPU yenye speed ya 1.8 GHz ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 ambao unaweza kuongezewa na memory card hadi ya GB 400. Sifa nyingine za LG Q8 (2018) ni kama zifuatazo.

Sifa za LG Q8

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~389 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.6 GHz Cortex-A53, Qualcomm SDM450 Snapdragon 450 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – GB 4
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye PDAF na LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3300 mAh battery battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging).
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Type-C 2.0 reversible connector, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Aurora Black, Moroccan Blue.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Bei ya LG Q8 (2018)

Kwa upande wa bei LG Q8 inakuja ikiwa inauzwa Won ya Korea ya Kusini KRW539,000 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,095,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.