Jinsi ya Kudownload WhatsApp Status kwa Kutumia Kompyuta

Njia nyingine ya kudownload WhatsApp stutus kwa kutumia kompyuta yako
Download whatsapp status Download whatsapp status

Wote tunajua kuwa WhatsApp inayo sehemu mpya ya Status ambayo kwasasa inakuja juu sana kutokana na kuongezaka kwa watumiaji wa sehemu hiyo, lakini kutokana na sehemu hiyo kuwa maarufu basi hata watu wanatafuta njia mbalimbali za kutumia sehemu hiyo kwa utofauti.

Hivi karibuni kumekuwa na njia nyingi pamoja na programu mbalimbali za kuweza kudownload picha na video ambazo zina kuwa kwenye WhatsApp Status. Lakini kuwa na programu nyingi kwenye simu yako kunaweza kusababisha simu kuwa slow na kuisha chaji haraka hivyo basi, kama hutaki kuwa na programu nyingi kwenye simu yako basi njia hii itakusaidia kudownload status ya mtu bila kutumia app au programu yoyote.

Kwa kuanza ni vyema kujua kuwa njia hii ni maalum kama unayo kompyuta, hivyo kama huna kompyuta basi unaweza kuendelea kutumia programu kwani kwa sasa bado hakuna njia ya kudownload picha na video za whatsapp status kwa kupitia simu bila kutumia App au programu maalum.

Advertisement

https://www.youtube.com/watch?v=Sn4DCsXlo48

Baada ya kusema hayo basi ingia kwenye kompyuta yako, kisha washa WhatsApp Web kwa kutembelea link hii web.whatsapp.com/?/en kisha fungua programu yako kwenye simu kisha bofya vidoti vitatu kwenye kona juu upande wa kulia kisha chagua WhatsApp web kisha itafungua kamera yenye box katikati kisha scan code yako kisha utaweza kutumia whatsapp kwenye kompyuta kisha bofya sehemu mpya ya status.

Bofya jina au status ya mtu unayetaka kudownload kisha baada ya picha kusoma vizuri basi bofya kitufe cha kulia (Right Click) kwenye mause ya kompyuta yako kisha chagua Save image As kama ni picha na chagua Save Video As kama ni video.

Baada ya hapo utakuwa umefanikisha kudownload WhatsApp status kwa kutumia kompyuta yako, njia hii ni rahisi na inaweza kukusaidia kunusuru simu yako kwa kuweka programu nyingi sana ambazo baadae zinaweza kusababisha simu yako kuwa slow kama inayo ram ndogo.

Lakini kama unataka kudownload status kwa kupitia simu hizi ni baadhi ya programu ambazo zinaweza kukusaidia kufanya hivyo kupitia simu yako ya Android.

  • Story Saver for Whatsapp
  • Status Downloader for Whatsapp

Na hizo ndio app ambazo utaweza kutumia kudownload status za whatsapp unaweza kupata app nyingi kupitia Play Store tafuta tu “WhatsApp Status Download” na utaona programu nyingine nyingi za kuweza kukusaidia kufanya kazi hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use