in

Programu Zinazoweza Kukupatia Kipato Kupitia Simu Yako

Kama unataka kutengeneza kipato kupitia simu yako ya Android au iOS soma hapa

kupata pesa kupitia app

Kutokana na ongezeko la watumiji wa simu za mkononi maarufu kama smartphone wafanya biashara nao wameanza kugeuza aina zao za biashara kuhamia kwa watumiaji wa simu hizo maarufu za mkononi,

Hivyo basi kutokana na hilo leo Tanzania Tech tunakuletea app au programu ambazo unaweza kutumia ili kupata kipato kwa kutumia simu yako ya mkononi yaani smartphone. Bila kupoteza muda basi twende tukaangalie programu hizo ambazo na hakika ukizingatia unaweza kuanza kujipatia kipato mara moja na kuendesha maisha yako ya kila siku.

3. Bitwalking

Bitwalking ni aina mpya ya programu ambayo inaweza kukutengenezea kipato kwa kuendelea na maisha yako ya kila siku.. ndio sijakosea…kama wewe ni mtu ambaye unatembea sana app hii itakuwa chaguo bora sana kwako na itakamilisha ule msemo unaosema “mtembea bure sio sawa na mkaa bure..”

  • Jinsi Inavyofanya Kazi

Mtumiaji atalipwa pesa kwa kutembea na app hiyo itarekodi umbali unaotembea na pale unapofikisha umbali wa hatua 10,000 basi utaweza kulipwa kiasi cha dollar 1 (moja), unaweza kulipwa kupitia akaunti yako ya bank lakini kumbuka bado programu hii ipo kwenye majaribio hivyo inaweza kuwa na mabadiliko yoyote.

Bitwalking BETA
Price: Free

2. miPic

Sidejoy ni app ambayo inaweza kukuletea kipato kwenye simu yako ya Android kwa kutumia simu yako ya iPhone kirahisi tu na unaweza kuendelea tu kutumia simu yako na utajipatia kipato ilimradi uwe mtaalamu wa kupiga picha

  • Jinsi Inavyofanya Kazi

App hii ni tofauti kidogo kwani unatakiwa kuwa mtaalamu wa kupiga picha na baadae utaweza kupewa kazi mbalimbali ambazo zitaweza kukusaidia kupata kipato baadae utakapo kuwa mtaalam. App hii kwa sasa inapatikana kwenye mfumo wa iOS pekee lakini unaweza kutumia tovuti yake hapa www.mipic.co kama utakuwa wewe ni mtumiaji wa Android.

‎miPic
Price: Free

1. Foap

Foap ni app ambayo hata mimi nimekua nikitumia kwa muda sasa na app hii itakupa uwezo wa kupata kipato kama wewe ni mpiga picha mzuri, kumbuka unatakiwa kutumia smartphone yako na unatakiwa kuwa na uhakika wa picha yako yani hati miliki.

  • Jinsi Invyofanya Kazi

Unatakiwa kuwa na simu yenye kemara nzuri kwani kwa kutumia app hii utaweza kuuza picha yako hiyo kuwa kiasi cha mpaka dollar 10. App hii pia inakuapa uwezo mbalimbali wa kufanya baadhi ya kazi za kupiga picha ambapo unaweza kujipatia mpaka kiasi cha dollar 100. App hii inapatikana kwenye mifumo yote ya Android na iOS.

Foap – Android

Foap – iOS

Na hizo ndio baathi tu ya programu au application ambazo unaweza kuzitumia kutengeneza kipato kwa kutumia simu yako ya mkononi maarufu kama smartphone, kumbuka huu sio mwisho wa list hii tutaendelea kukuwekea programu nyingine nyingi kwenye ukurasa huu hivyo akikisha unapitia ukurasa huu kila siku kujua programu mpya iliyo ongezwa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Programu Muhimu Kuwa Kwenye Kompyuta (Windows)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

41 Comments

  1. Pia waweza jaribu hii ili kujiongezea kipato cha ziada mtandaoni. Jisajiri na buddytraveller kisha share link yako kwa marafiki na kila atakaejisajiri kupitia hiyo link atakuwezesha kuingiza kipato…ingia na ujisajiri kupitia link hii