LG V20 Hii Ndio Simu Bora Kuliko Zote Kutoka Kampuni ya LG

Kampuni ya LG hiv karibuni ilitoa simu yake ambayo pengine ndio simu bora kuliko simu nyingine kutoka kampuni hiyo
LG V20 LG V20

Kama wewe ni mpenzi wa simu kutoka kampuni ya LG lazima utakua unaijua simu mpya ya LG V20, lakini kama kwa bahati mbaya wewe huijui simu hiyo basi endelea kusoma makala hii kwani nakuhakikishia ukimliza kusoma makala hii utakubaliana na mimi kuwa LG V20 ndio smartphone ambayo ni bora sana kutoka kwenye kampuni hiyo.

Kwa kuanza binafsi yangu lazima niwe mkweli, na ukweli wenyewe ni kwamba sijawahi kupenda smartphone yoyote kutoka kampuni ya LG mpaka nilipo ona simu hii mpya ya LG V20, kama unajiuliza sababu ni nini mpaka nilikua sipendi simu janja za LG basi bila shaka naamini ya kuwa kila mtu anayo maoni yake binafsi linapokuja swala zima la smartphone ipi ni bora na kwa sababu gani. Lakini leo nauhakika ukimaliza kusoma makala hii utakubaliana na mimi kuwa LG V20 ndio Smartphone bora pengine kuliko simu nyingine zilizopita kutoka kampuni ya LG.

Baada ya kusema yote hayo sasa twende tukaangalie kwanini nasema LG V20 ni simu bora kuliko simu nyingine kutoka kampuni ya LG.

Advertisement

  • Hardware (Ubora wa ndani ya Simu Hii)

Kwenye toleo hili la LG V20 kampuni ya LG imeweka nguvu kubwa sana kutengeneza simu hii kwa teknolojia za hali ya juu sana. Simu hii mpya ya LG imetengenezwa kwa kava la titan pamoja na silver ikiwa na uwezo mkubwa wa kuzuia michubuko pale simu yako inapo anguka, mbali na hayo simu hii mpya ya LG V20 inayo kioo bora cha inch 5.7” Quad HD Display chenye kutumia teknolojia ya IPS ambayo inauwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya milioni 16.

Pia simu hii mpya inayo kamera mbili kwa nyuma zenye uwezo wa 16 Mega Pixel kila moja zenye uwezo wa kupiga picha kwa Angel tofauti kila moja, kamera hizo pia zinatumia teknolojia ya Steady Record 2.0 ambayo inakuwezesha kuchukua video hata kama uko kwenye mwendo bila picha kuchezacheza.

Kwa upande wa sauti simu hii mpya ya LG bado inatumia sehemu ya earphone jack (pini) ambayo inauwezo wa kutoa sauti bora sana hata kama unatumia earphone zenye nguvu sana, simu hii imetengenezwa kwa teknolojia ya juu sana kwani inatumia Hi-Fi Quad DAC pamoja na Hi-Fi Video Recording ambayo inakupa uwezo wa kurekodi sauti bora sana unapo chukua video au kurekodi sauti ya kawaida.

Pia kingine kipya kwenye simu hii mpya ya LG ni kwamba kwenye kioo chake kwajuu simu hii inayo kioo kidogo ambacho kinakupa uwezo wa kupata sehemu kama za kuwasha bluetooth, wireless, touch au hata kuwasha programu mbalimbali ikiwa pamoja na settings.

https://www.youtube.com/watch?v=88RB4qKWP50

  • Software (Programu za Ndani za Simu Hii)

LG V20 imetengenezwa kwa programu bora na mpya ambazo zinafanya matumizi ya simu hii kuwa marahisi na ya kisasa zaidi, simu hii mpya imekuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android Nougat 7.0 ambao una sehemu nyingi mpya zinazofanya simu hii iwe bora na ya kisasa.

Simu hii ndio moja ya kati ya simu ambazo ni za kwanza sana kupata mfumo huo mpya zikifatiwa na simu nyingine ambazo zinategemewa kupata mfumo huu wa Android Nougat 7.0 kwenye miezi inayokuja.

Je unasemaje kuhusu simu hii mpya kutoka LG..? unaweza kuandika maoni yako hap chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store

8 comments
    1. Asante emma kwa kutembelea tanzania tech. (RAM ni 4Gb) Hizo hapo juu sio sifa za simu hiyo bali ni sababu kwanini hiyo simu ni bora kuliko zingine kutoka LG, kuhusu ROM nadhani tumeandika hapo juu kuwa simu hiyo inatumia Android 7.0

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use