Elewa Kuhusu Teknolojia Mpya ya 4K Kwenye TV

4k TV 4k TV

Watu wengi hujiuliza nini maana ya 4K hasa ikija katika swala zima la televisheni, basi bila shaka leo tutaenda kujua nini maana ya teknolojia hii mpya ya 4k, kwa kuanza basi labda tuende tukajue. Je 4K ni nini..?

4K ni neno la kiteknolojia linalotumika kuelezea kuhusu kioo cha tv chenye mkusanyiko wa jumla wa pixel ambao ni mara 4 zaidi ya pixel zinazopatikana kwenye kioo cha tv yenye Full HD.

Televisheni ya 4K haina haja ya kuwa na pixel 4,000+ kwa usawa (Horizontal) ili kuwa na teknolojia ya 4K hii ni kutokana na tv nyingi zenye teknolojia hii ya 4K zinayo uangavu wa kioo (Resolution) wa 1920 x 1080p ambapo hii ni zaidi ya 4,000+ pixel kwa usawa kwenye tv za kawaida zenye full HD.

Advertisement

Mara nyingi televisheni hizi uja na muundo wa aina tofauti kuna zile zinazokuja zikiwa zimejikunja kidogo (Curved) na kuna zile ambazo zinakuja zikiwa zina usawa yaani (Flat Screen).

Zaidi ni kwamba 4K tv ni zaidi ya unavyo tegemea kwani tv hizi nyingi zainakuja zikiwa na teknolojia nyingi mbalimbali ambazo zinafanya uone tv yako kuwa nzuri zaidi kwa mfano tv hizi nyingi zinakuja na teknolojia ya kuweza kungarisha video za kawaida hata kama hazina teknolojia ya 4K, kwa kutumia teknolojia hii una uwezo wa kubadilsha video na picha za kawaida kua angavu zaidi.

Hata hivyo watu wengi huchanganya katika hili kwani ili kupata muonekano angavu unaotakiwa wa 4K  ni lazima video au picha unayotaka kuangalia iwe imechukuliwa na kifaa chenye teknolojia ya 4K , kwa mfano iPhone 7 na nyinginezo.

Pia imesika watu wengi wakibisha sana kuhusu tv zenye teknolojia ya 4K na UHD ukweli ni kwamba kuna tofauti kidogo kwenye hili hasa ikija katika maswala ya kitekonlojia kwani tv zenye teknolojia ya UHD zinauwezo wa kuonyesha picha ambayo ni nusu ya teknolojia ya 4K inavyo onyesha, kifupi ni kwamba UHD ni teknolojia mbayo bado haija fikia kwenye kiwango cha 4K Angalia picha hii kuelewa zaidi.

Digital_video_resolutions_(VCD_to_4K).svg

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka,pia kwa kujifunza mambo mablimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use