Jinsi ya Kubadilisha Video Yoyote Kuwa Video ya Katuni 1

Jinsi ya Kubadilisha Video Yoyote Kuwa Video ya Katuni

Katika hali ya kawaida ni wazi kuwa kuna wakati unahitaji kuedt video zako kwa namna ya kipekee na kufanya ziwe tofauti na video za watu wengine. Kuliona hili leo Tanzania tech tumekuletea njia mpya ambayo itakusaidia kubadilisha video yoyote kuwa na muonekano kama video ya katuni.

Njia hii inafanya kazi vizuri sana, lakini kwa sasa unaweza kubadilisha video fupi kuwa na muonekano wa katuni. Kitu cha muhimu hakikisha simu yako au kompyuta inayo Internet kisha moja kwa moja tembelea link hapo chini na moja kwa moja chagua sehemu ya video na hakikisha video yako haizidi MB 30.

Jinsi ya Kubadilisha Video Yoyote Kuwa Video ya Katuni 2

Baada ya kuweka video yako subiri baada ya muda mfupi moja kwa moja utaweza kudownload video yako ikiwa na muonekano wa katunia. Njia hii inafanyakazi kwenye video nyingi ila kuna baadhi ya video inaweza isifanye kazi kwa usahihi kwa asilimia 100. Unaweza kujaribu video yako hapo chini.

Badilisha Video Yako Hapa

Kama unataka kujaribu kubadilisha picha yoyote kuwa na muonekano wa katuni, unaweza kusoma hapa kujua hatua kwa hatua jinsi ya kufanya hivyo.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Jinsi ya Kupata Namba ya Simu ya Nje ya Nchi Bure 3
Jinsi ya Kupata Namba ya Simu ya Nje ya Nchi Bure
Next Post
Jinsi ya Kupokea SMS Kwenye Barua Pepe (Email) 4

Jinsi ya Kupokea SMS Kwenye Barua Pepe (Email)