Kwa sasa nadhani karibia Tanzania nzima wananchi wote wanatumia Luku kupima kiwango cha matumizi ya umeme wa kila siku, Matumizi haya ya Luku yamebadilisha kabisa jinsi tulivyokuwa tunatumia umeme hapo awali kwa maneno mengine ni kwamba kwa sasa watu wengi wanaonekana kutumia umeme kwa ustaarabu mkubwa kuliko hapo awali kwani mfumo huu wa Luku umeleta mipango ya kutumia kadri unavyo nunua na nunua kadri unavyotumia.
Mipango hii ndio inyofanya leo niandike makala hii kwani watu wengi sana wanao kaa kwenye nyumba za kupanga ndio wanaoadhirika sana na mipango hiyo. kwa mfano kuna wakati unakuta labda wewe huna kitu ndani kwako lakini pesa unayoambiwa uchangie pengine ni kubwa kuliko matumizi yako hivyo unakuta mfumo wa kulipia kadri unavyotumia unakuadhiri moja kwa moja. Lakini kama haitoshi pengine wewe ni mtu ambaye ushindi nyumbani hivyo unakuta hela unayotoa kununua umeme haifikishwi yote na unakuta umeme unao-wekwa ni mdogo kuliko dhamani ya pesa yako uliyo toa hivyo unakuta unalipa zaidi ya unavyotumia na pengine pesa uliyotoa kununua umeme huo si sawa na kiwango cha unit kilichowekwa.
Basi kama wewe ni mmoja wa watu hao endelea kusoma makala hii kwani mpaka mwisho wa makala hii utaweza kujua namna ya kuangalia kiwango cha mwisho kilichowekwa kwenye mita yako ya Luku ikiwa ni moja kwa moja kwenye mita yako hiyo. Kwa kuanza basi nadhani kila mtu atakua anaijua mita ya Luku jinsi ilivyo pamoja na muonekano wake pale unapo ingiza tarakimu ili kuweka umeme, pia najua mita zinatofautiana lakini naimani njia hii inafanya kazi karibia kwa kila mita za Luku ambazo zinatumia vibonyezo vya namba.
Basi kama mita yako iko hivyo moja kwa moja ili kuangalia kiwango cha umeme kwenye mita yako hakikisha kuna umeme kisha bofya namba 2 pamoja na kibonyezo cha kuweka umeme (Enter) hakikisha unabonyeza vyote kwa pamoja kisha achia.

Baada ya hapo utaona namba za kwanza ambazo ndizo zinaonyesha kiwango cha umeme kilicho wekwa kwa mara ya mwisho kwenye mita yako ya Luku, hakikisha unaangalia namba za kwanza zinazo anza kutokea kwenye kioo cha mita yako kwani namba hizo hubadilika na baadae baada ya kama sikunde 3 namba hizo hurudia hali yake ya awali na kuendelea kuhesabu kiwango cha umeme uliopo hivyo kama utakua ujaona vizuri basi subiria namba hizo zirudi kwenye hali yake alafu urudie tena kufanya hatua hizo.
Angalizo : Njia hii ni salama kabisa lakini kumbuka Mita ya Luku ni mali ya Tanesco hivyo ni vyema kufanya hatua hizi kwa uangalifu usije kuharibu au kubadili chochote kwenye mfumo wa mita yako.
Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kungalia kiwango cha mwisho kilichowekwa kwenye mita yako ya Luku kama una maswali unaweza kuuliza kupita hapa kama una maoni au ushauri unaweza kutuandikiwa hapo chini na ili kupata habari zote za teknolojia endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.


