Tigo Tanzania Yabadilisha Jina Sasa ni “YAS”

Hii sio mara ya kwanza kwa Kampuni hii kubadilishwa jina ilikuwa Mobitel (BUZZ), kisha TIGO na sasa ni YAS!
Tigo Tanzania Yabadilisha Jina Sasa ni "YAS" Tigo Tanzania Yabadilisha Jina Sasa ni "YAS"

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania imebadilisha jina lake na sasa inajulikana kama YAS. Mabadiliko haya yanaashiria hatua mpya katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano nchini, ambapo kampuni hiyo inalenga kuboresha huduma zake na kuendana na mahitaji ya kisasa ya wateja.

YAS imetangaza mabadiliko ya jina kwenye bidhaa yake ya TIGO PESA ambayo kuanzia leo itakuwa ikiitwa MIXX BY YAS.

Advertisement

Mabadiliko haya yametangazwa na Uongozi wa Kampuni hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Dar es salaam leo mchana ambayo Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kampuni hii kubadilishwa jina katika miaka yake yote thelathini ya huduma Nchini Tanzania ambapo awali ilikua ikiitwa Mobitel (BUZZ), kisha TIGO na sasa ni YAS!

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *