Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apple Yatoa Mfumo Mpya wa iOS 12 (Download Hapa Sasa)

Kama unayo moja ya vifaa hivi Download hapa mfumo wa iOS 12
mfumo wa iOS 12 Download mfumo wa iOS 12 Download

Kampuni ya Apple hivi karibuni imezindua simu zake mpya za iPhone, katika uzinduzi wa simu hizo Apple pia ilitangaza rasmi kuwa mfumo wa iOS 12 unatarajiwa kutoka rasmi hivi karibuni.

Hadi kufikia siku ya leo tayari toleo la iOS 12 limeshatoka rasmi na sasa unaweza kusasisha (update) mfumo huo moja kwa moja kwenye kifaa chako chenye uwezo wa kupokea mfumo huo. Kama wewe unatumia vifaa vifuatavyo basi unaweza kusasisha toleo hilo moja kwa moja.

Advertisement

iPhone Zenye Uwezo wa Kupokea iOS 12

  • iPhone X
  • iPhone 8
  • iPhone 8 Plus
  • iPhone 7
  • iPhone 7 Plus
  • iPhone 6s
  • iPhone 6s Plus
  • iPhone 6
  • iPhone 6 Plus
  • iPhone SE
  • iPhone 5s

iPad Zenye Uwezo wa Kupokea iOS 12

  • 12.9-inch iPad Pro 2nd generation
  • 12.9-inch iPad Pro 1st generation
  • 10.5-inch iPad Pro
  • 9.7-inch iPad Pro
  • 9.6-inch iPad
  • iPad Air 2
  • iPad Air
  • iPad 5th generation
  • iPad mini 4
  • iPad mini 3
  • iPad mini 2

iPod touch Zenye Uwezo wa Kupokea iOS 12

  • iPod touch 6th generation

Kama tayari unavyo moja ya vifaa hivi basi unaweza ku-update kifaa chako kwa kuingia kwenye sehemu ya Settings > General > Software Update, kisha subiri kidogo utaweza kuona mfumo huona kisha bofya Download and Install. Hakikisha simu yako inachaji ya kutosha kuanzia asilimia 50 au zaidi. Pia hakikisha simu yako inayo bando ya kutosha angalau GB 2 au zaidi.

Kama kwa namna yoyote umeshindwa ku-update kifaa chako kwa kutumia simu yenyewe unaweza kudownload mfumo huu wa iOS 12 kisha install kwa kutumia iTunes, unaweza kupata mfumo huo kwa kudownload kwa kutumia link hapo chini. Kumbuka hakikisha unadownload mfumo kulingana na kifaa chako.

Kama unataka kujua mabadiliko mapya yanayoletwa na mfumo huu mpya wa iOS 12 unaweza kusoma makala yetu hapa. Pia kama unaona kuna link ambayo haifanyi kazi unaweza kutuambia kwa kutuandikiwa kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use