Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Taariifa zinazofahamika tayari juu ya toleo lijalo la simu za Apple.
Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Kampuni ya Apple inatarajiwa kutoa simu zake mpya, toleo la iPhone 15 mwezi unaokuja. Japo bado takribani mwezi mzima hadi kuzinduliwa kwa simu hizo, tayari kuna taarifa mbalimbali juu ya sifa, mwonekano na uwezo wa simu hizo ambazo zimefahamika kutoka katika vyanzo mbalimbali, nyingi zikiwa zaq kuaminika.

Katika mengi yaliyo wekwa wazi tayari, haya ni matano ambayo ni muhimu, na ni mabadiliko kutokea kwenye toleo la mwaka jana, iPhone 14.

iPhone 15 Kutumia Waya wa Type-C

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Advertisement

Taarifa za awali zinaeleza ya kuwa Apple watatumia waya aina ya Type-C kwa ajili ya kuchaji na kuhamisha taarifa kwenye iPhone 15. Hii itakuwa ni mara ya pili Apple kubadilisha aina ya waya katika simu za iPhone tangu kuanza kuzitengeneza mwaka 2007.

Hadi mwaka jana, Apple walitumia waya aina ya Lightning, lakini kutokana na msukumo kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya, uliotaka kutumika kwa aina moja ya waya kwa ajili ya kundi kubwa la vifaa vya kielektroniki, Apple wamekosa namna, na kutakiwa kubadilisha aina hiyo.

Dynamic Island Kuja kwenye iPhone 15 Zote

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Apple wanatarajiwa kuileta Dynamic Island kwenye miundo yote ya iPhone 15, yaani iPhone 15, 15 Plus, 15 Pro na 15 Pro Max (ambayo huenda ikabadilishwa na kuitwa iPhone 15 Ultra). Walizindua hii mwaka uliopita, ambapo ilikuwa kwa miundo ya juu tu, yaani Pro na Pro Max.

Fremu ya Simu Kutengenezwa kwa Titanium

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Fremu za iPhone 15 zinatarajiwa kubadilishwa toka kwenye Chuma cha Pua (Stainless Steel) kuwa Titanium. Titanium inasifika kuwa imara zaidi huku ikiwa nyepesi zaidi ya Steel. Hili linategemewa kufanya simu za iPhone 15 kuwa na uimara zaidi.

Ongezeko la Ukubwa wa Betri

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Betri za matoleo yote ya iPhone 15 zinasemekana kuongezwa ukubwa kwa asilimia 12 hadi 18 ukilinganisa na betri za matoleo ya iPhone 14, Hii kwa kujumuisha na uwepo wa chipset mpya kwa simu hizo inatarajiwa kuongeza muda wa matumizi wa simu pakubwa, kwa kulinganisha na matoleo ya iPhone 14.

Kutolewa kwa Swichi ya Miundo ya Sauti

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Swichi maarufu ya miundo ya Sauti (Alert Slider) ilioko juu ya vitufe vya kuongeza na kupunguza sauti inasadikika kutolewa, na badala yake, Apple wataweka kitufe maalumu (Action Button) kama kwenye saa yao aina ya Apple Watch Ultra. Mtumiaji wa simu ataweza kubadili matumizi ya kutufe hicho kulingana na mahitaji yake, ikiwemo kubadili miundo ya sauti ama kufungua programu anayoitaka haraka zaidi

Pamoja na hayo, mengine ni kama kupungua kwa mistari inayozunguka kioo (bezels), maboresho ya kamera, na mabadiliko ya chipset. Yote haya yatafaham,ika kwa undani haswa simu hizo zitakapozinduliwa, mwishoni mwa mwezi Septemba.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use