Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Fahamu bei ya Redmi Note 13, Note 13 Pro pamoja na Redmi Note 13 Pro 5G
Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13 Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Kampuni ya Xiaomi inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki zikiwemo simu za mkononi imetaja bei za simu zake mpya za Redmi Note 13 nchini Tanzania zilizo zinduliwa hivi karibuni.

Bei ya Simu Mpya za Redmi Note 13

Xiaomi imesema imekuja na matoleo tofauti ya simu hizo ili kuwafanya wateja wake wa madaraja yote kuwa na uwezo wa kumiliki simu hizo.

Advertisement

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Xiaomi Redmi Note 13

Kwa Redmi Note 13 yenye RAM ya GB 6 na uhifadhi wa GB 128 inauzwa kuanzia TZS 469,000 hadi TZS 509,000. Kwa Redmi Note 13, yenye RAM GB 8 na uhifadhi wa GB 256 unaweza kupata kwa kuanzia TZS 559,000.

Xiaomi Redmi Note 13 Pro

Kwa upande wa Xiaomi Redmi Note 13 Pro yenye GB 8 na uhifadhi wa ndani wa GB 256 utaipata kuanzia TZS 719,000. Hata hivyo kama unahitaji RAM na Storage zaidi basi unaweza kupata Redmi Note 13 Pro yenye RAM GB 12 na uhifadhi au Storage GB 512 kwa kuanzia TZS 849,000.

Xiaomi Redmi Note 13 Pro 5G

Kwa upande wa simu zenye kasi ya 5G ambazo ni Redmi Note 13 Pro 5G utaweza kupata GB 8 za RAM na GB 256 za uhifadhi wa ndani au Storage kuanzia TZS 1,029,000, pia kama unahitaji storage zaidi unaweza kununua toleo lenye RAM GB 12 na Storage GB 252 kwa TZS 1,159,000.

Muundo na Mabadiliko Zaidi

Matoleo hayo ya Redmi Note 13 yanakuja katika rangi tofauti zikiwemo nyeusi, nyeupe, zambarau, kijani na bluu.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Simu hizo zinakuja na maboresho makubwa kwenye kwenye mifumo wa kamera na betri (5000mAh) zenye uwezo wa kuhifadhi nishati kwa muda mrefu.

Maboresho mengine kwenye matoleo hayo ni pamoja na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi wa simu unaozipa uwezo wa kufanya kazi kwa kasi bila kukwama-kwama.

Redmi Note 13 zina vioo vyenye picha ang’avu lakini pia zina chaguo la kutumia mwanga wenye kulinda macho huku zikiwa na muonekano mzuri wa nje na zinazovutia watumiaji.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Sambamba na uzinduzi wa simu hizo, Xiaomi pia imetambulisha saa zake ambazo zina uwezo wa kuunganisha mawasiliano katika simu zake.  Saa hizo ni Redmi Watch 4, Redmi Buds 5 Pro na Redmi Buds 5.

Saa hizo za kisasa zinamfanya mtumiaji wa simu kuwa na uwezo wa kupokea simu na kusoma jumbe zinazoingia kwenye simu bila kushika simu.

Pia zina uwezo wa kupima mapigo ya moyo pamoja na oxyjeni kwenye damu ikiwa ni pamoja na kuonyesha muda ambao mtumiaji amesimama au kukaa na kumshauri kukaa kama amesimama kwa muda mrefu na  kusimama kama amekaa kwa muda mrefu.

Redmi imewataka wateja wake kutembelea tovuti yake rasmi ili kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bidhaa zake ili kuepuka utapeli wa bei na bidhaa zisizo na viwango.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use