Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2

Ni Apple Watch Series 9 pamoja na Apple Watch Ultra 2
Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2 Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2

Ukiachana na simu mpya za iPhone 15 zilizotangazwa hapo juzi, Apple pia walitangaza saa janja (smart watches) mpya kutoka kwao. Apple walitangaza saa mbili, Watch Series 9 na Watch Ultra 2. Saa hizi ni maboresho kutoka kwenye Matoleo yaliyopita ya Series 8 na Watch Ultra. Kila Saa imefanyiwa mabadiliko kadhaa, nayo tutayatazama kama ifuatavyo.

Apple Watch Series 9

Kwa mpangilio wa sasa wa matoleo ya saa janja kutokea Apple, hili ni toleo la kati, likiwa juu ya Watch SE na chini ya Watch Ultra, sasa Watch Ultra 2. Saa hii janja inaleta maboresho katika sehemu mbalimbali.

Advertisement

Suala la msingi kabisa ni kuwa Saa janja hii inakuja na chip mpya ya kuiendesha kutokea Apple iitwayo S9. Chip hii itaboresha ufanyaji wa saa hii, kuifanya kuwa na mfumo nyororo zaidi huku saa ikiw ana muda wa matumizi wa takribani masaa 18.

Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2

Pia, Watch Series 9 inakuja na skrini yenye uangavu zaidi, pamoja na uwezo wa kuchakata amri unazoipa Siri ndani ya Saa bila kuhitaji internet. Kwa Saa hii, Apple pia wa,eomgeza uwezo wa kuitafuta simu yako ya iPhone ama ya mwingine kwa urahisi na uhakika zaidi.

Apple pia wameongeza uwezo wa kupima mazoezi kwa waendesha baiskeli, ambapo sasa mtu ataweza kuona kasi pamoja na taarifa nyingine kumhusu kupitia saa yake. Taarifa hizi pia zitaonekana kwa urahisi kupitia app ya afya ya Apple katika simu za iPhone.

Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2

Pengine, suala kubwa lililozinduliwa na saa hizi ni matumizi ya ishara mkono katika kuiendesha na kuitaarifu saa kufanya vitu kadhaa. Kupitia sensors za Watch Series 9, sasa mtumiaji ataweza kugusanisha kidolle gumba na kinachofuata ili kufungua programu ama shughuli fulani katika saa, namna mtumiaji atakavyotaka.

Apple Watch Ultra 2

Mnamo mwaka jana. Apple walizingua Watch Ultra, ikiwa imelenga watu wenye matumizi yaliyo na uhitaji wa uimara zaidi na uwezo mkubwa wa kukaa na chaji. Watch Ultra ilipokelewa vyema, licha ya kuwa na bei kubwa, na Watch Ultra 2 ni mwendelezo wa toleo hilo.

Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2

Katika toleo hili la Pili, Apple wameipa saa hii janja maboresho kama ya S9, ikiwa ni Chip mpya, uwezo wa matumizi kwa ishara za mkono, uwezo wa kutafuta simu yako ama simu nyingine kwa urahisi, maboresho ya matumizi ya mfumo wa Siri katika saa na upimaji wa mazoezi.

Lakini, kimaalumu kabisa kwa saa hii ya Watch Ultra 2, Apple wameongeza uangavu wa skrini yake na kufikia kiwango cha Nits 3000, ikiwa ni mojawapo ya viwango vikubwa zaidi vya uangavu duniani kwa saa, hata kwa simu pia (kama sio kiwango kikubwa zaidi). Pia Apple wameweka mwonekano uitwao “Modular Ultra” ambao utabeba taarifa zaidi kuonekana kwa mara moja katika skrini. Bado, saa hii itakuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa masaa 36, ikifikisha masaa 72 ikiwa imewekw katika muundo wa nguvu kidogo.

Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2

Katika matoleo yote ya saa mwaka huu, Apple pia walitumia muda kueleza namna ambavyo saa janja zao kwa mwaka huu zimekuwa bidhaa za kwanza kutoka Apple kufikia lengo la kupunguza kaboni (Carbon Neutral) kwa asilimia 100, kupitia kutumia malighafi zilizotumika hapo kabla, kubadili mifumo yao ya uzalishaji, usafirishaji na ubunifu katika malighafi wanazotumia.

Watch Series 9 itagharimu Dola za Kimarekani $399 (Sawa na Shilingi za Kitanzania takribani TZS 999,740/-) na Watch Ultra 2 itagharimu Dola za Kimarekani 799 (Sawa na Shilingi za Kitanzania takribani 2,002,000/-) Saa zote zimeanza kuagizwa tangu Jumanne, na zitaanza kupatikana Ijumaa ijayo, Tarehe 22/09 ( Tutegemee kuchukua muda kidogo zaidi kufikia nchi yetu ya Tanzania)

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use