Sasa Kupitia WhatsApp Unaweza Ku-Forward Meseji Tano tu

Badala ya watu ishirini (20) sasa utaweza ku-forward kwa watu watano (5) tu
Kuforward meseji WhatsApp Kuforward meseji WhatsApp

Hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa kusambaa kwa habari zisizo za ukweli kupitia app ya WhatsApp, habari hizo zimekuwa zikisambaa kwa urahisi sana kwa kutumia sehemu ya Forward inayopatikana ndani ya programu ya WhatsApp. Sasa kuliona hilo hivi karibuni whatsapp imekuja na sheria mpya ya kuzuia idadi ya meseji unazoweza ku-forward ndani ya programu hiyo.

Kwa mujibu wa habari kutoka Android Authority, hivi karibuni watumiaji wa matoleo mapya ya programu zote za WhatsApp kote duniani wataruhusiwa ku-forward meseji kwa watu wa tano tu kwa wakati mmoja. Inasemekana kuwa sheria hiyo mpya itaanza kutumika hivi karibuni ili kuzuia kusambaa kwa habari zisizo za ukweli ambazo zimekuwa zikisambaa sana kwa kutumia app hiyo.

Hapo awali sheria hii ilikuwa ikitumika kwa nchini India pekee, huku nchi nyingine zilikuwa zikiruhusiwa ku-forward meseji hadi kwa watu 20. Kwa sasa mambo yamebadilika kwani sheria hiyo ya nchini india itakuwa inatumika kwa watumiaji wa WhatsApp dunia nzima.

Advertisement

Hivi karibuni tovuti ya BBC ilitangaza kuwa programu ya WhatsApp inahusika kusababisha vifo vya watu zaidi ya 25 nchini India, huku vifo hivyo vikisemekana kusababishwa na kusambaa kwa habari zisizo za ukweli (Fake News) zinazo sambaa kupitia programu hiyo.

India na Brazili ni moja kati ya nchi ambazo zinasemekana kuwa na idadi kubwa ya watu wanao adhiriwa na kusambaa kwa habari feki, huku idadi hiyo ikisemekana kupungua kutokana na ujio wa sehemu mpya zinazo zuia watu kusambaza habari feki kwa kutumia app hiyo.

Kwa sasa bado hakuna taarifa lini sheria hii mpya itanza kufanya kazi, lakini kwa mujibu wa tovuti mbalimbali huenda sehemu hiyo ikaanza kufanya kazi kabla ya mwisho wa mwezi huu January.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use