Apps Nzuri za Kusaidia Ku-forward Meseji Kwenye Simu Yako

Apps hizi pia zinaweza kusaidia kusoma meseji za mtu kwa urahisi
apps za kusoma meseji za mtu apps za kusoma meseji za mtu

Linapokuja swala la SMS ni wazi kuwa teknolojia hii inaenda ikipitwa na wakati, lakini kutokana na teknolojia hii kupitwa na wakati imekuwa ni ngumu sana kufanya mambo mbalimbali kwenye SMS kama vile ku-forward meseji pamoja na mambo mengine.

Kuliona hili leo nimekuletea list ya App nzuri ambazo unaweza kuzitumia ku-forward meseji kwenye simu yako. App hizi zitakusaidia kwenye nyakati mbalimbali kwa mfano, unaweza ukawa unachaji simu yako moja na ungependa kutoka kuiacha kwenye chaji, kwa kutumia app hizi utaweza kuendelea kupokea meseji zako kwenye simu yako nyingine hata kama umeacha simu hiyo kwenye chaji. Sio hayo tu, apps hizi nzuri zinaweza hata kusaidia wale wenye wivu wa mapenzi….

Anyway kwa kuwa lengo ni kujifunza na sio vinginevyo basi tusipoteza muda wako twende moja kwa moja tukangalie apps hizi nzuri.

Advertisement

Auto SMS Lite(Autoresponder)

Auto SMS Lite ni app nzuri sana kwani inaenda kukusaidia zaidi ya ku-forward meseji, app hii inaenda kukupa uwezo wa kujibu meseji bila kushika simu yako na pia itakusaidia kuweza kutuma meseji kwa wakati fulani hataka kama hujashika simu yako. App hii ni nzuri sana na kama wewe bado unatumia SMS mara nyingi basi download app hii kupitia link hapo chini.

PhoneLeash: SMS/MMS forwarding

Phone Leash ni app nyingine nzuri ambayo unaweza kuforward meseji kwa haraka. App hii nayo ni nzuri sana kwani inakupa uwezo wa kufanya mambo mengi zaidi ya ku-forward meseji, kwa kutumia app hii unaweza kujibu meseji au SMS kwa kutumia barua pepe yako kama gmail, yahoo na nyingine. Unaweza kudownload app hii kwa kubofya hapo chini.

Message Forwarder

Message Forwarder ni app nyingine nzuri sana ya kusaidia ku-forward meseji, app hii inakupa uwezo kupokea meseji kutoka kwenye namba nyingine na uzuri ni kwamba unaweza kupokea meeji hizo kwa kutumia simu au kwa kutumia barua pepe. Unaweza kupakua app hii kupitia link hapo chini.

SMS Call Forward / Divert

App hii ni nzuri sana kwa wale ambao wanapenda ku-forward SMS lakini pia kwa wale wanaopenda ku-forward simu au Call. App hii itakusaidia kurahisha mawasiliano kutoka kwenye simu yako moja kwenda kwenye simu nyingine, unacho takiwa kufanya ni kudownload app hii kupitia link hiko hapo chini.

Forward SMS texting w/ 2phones

Forward SMS ni app nyingine nzuri ya kukusaidia kupa meseji kutoka kwenye simu yako au kutoka kwenye simu ya mtu mwingine kuja kwenye simu yako, app hii inauwezo wa kuchukua meseji pamoja na simu zinazo ingia kwenye simu ya mtu na kuzileta kwenye simu yako mara moja. Unaweza kupata app hii kupitia link hapo chini.

Na hizo ndio apps nzuri nilizo kuandali kwa siku ya leo, kama una maswali au kuna mahali umekwama unaweza kuuliza kupitia hapo chini. Kama unajua apps nyingine nzuri za ku-forward meseji kwenye simu unaweza kutujuza kupitia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Kama unataka kujua apps nyingine nzuri za kuangalia mpira wa miguu kwenye simu yako unaweza kusoma makala yetu iliyopita kupitia hapa, kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

7 comments
  1. Kwa mfano nataka kuinstall app kwenye simu ninayotumia nipate sms za simu nyingine bila kuishika hiyo simu nyingine inawezekana?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use