Kutumia App ya WhatsApp kwa Lugha ya Kiswahili

Utaweza kubadilisha maandishi yote kwenye programu hiyo kuwa ya Kiswahili
WhatsApp kwa Kiswahili WhatsApp kwa Kiswahili

Programu ya WhatsApp ni moja kati ya programu zinazotumiwa na watu wengi sana kwa sasa, programu hii imewezesha watu kuwasiliana kwa urahisi, iwe ni watu kutoka nje au ndani ya Afrika.

Kurahisisha mawasiliano zaidi hivi karibuni mitandao mbalimbali ya kijamii imeanza kutambua Kiswahili kama lugha rasmi ya kuwasiliana ndani ya mitandao hiyo.

Kupitia programu ya WhatsApp ya Android sasa unaweza kubadilisha lugha ya programu hiyo moja kwa moja na utaweza kutumia programu hiyo ikiwa kwenye lugha adhimu ya kiswahili.

Advertisement

Kama unavyona kwenye picha hapo chini maneno yote kwenye programu hiyo yamebadilika na kuwa kwa lugha ya Kiswahili.

  • Jinsi ya Badilisha App ya WhatsApp Kuwa ya Kiswahili

Kama ulikuwa unataka kubadilisha programu yako ya WhatsApp ya Android kuwa ya kiswahili unaweza kufuata hatua hizi.

Kwanza hakikisha una update app yako ya WhatsApp kisha baada ya hapo fungua App hiyo kisha ingia kwenye Settings kisha chagua Chats.

Kutumia App ya WhatsApp kwa Lugha ya Kiswahili

Baada ya hapo moja kwa moja chagua sehemu ya App Language inayo patikana chini ya chat settings.

Kutumia App ya WhatsApp kwa Lugha ya Kiswahili

Kupitia sehemu hiyo bofya kuweza kubadilisha lugha ya programu ya WhatsApp na chagua Kiswahili.

Kutumia App ya WhatsApp kwa Lugha ya Kiswahili

Kwa kufanya hivyo programu ya WhatsApp itakuwa imebadilika na kuwa kwenye lugha ya Kiswahili.

Kwa kuwa lugha fasaha ya kiswahili ni ngumu kama unataka kurudisha WhatsApp kuwa lugha ya English basi unaweza kufanya hivyo kwa kuchagua sehemu ya Mpangilio > Soga > Lugha ya programu, badilisha na weka Lugha ya simu.

Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kubadilisha lugha ya programu yako ya WhatsApp kuwa Kiswahili. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuchat kupitia kwenye programu ya WhatsApp huku ukitembea.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use