Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Utaweza kuzuia bando lako kuisha kwenye simu yako kwa asilimia 100
Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android) Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la bei ya bando na hii imefanya watu kushindwa kufanya mambo mbalimbali mtandaoni kama walivyokuwa wanafanya hawali. Kuliona hili leo nimekutea njia bora ambayo inaweza kukusaidia kuzuia bando lako kuisha kwa haraka.

Njia hii ni bora na nauhakika itakusaidia sana hasa kama umekuwa ukikumbana na tatizo la bando kuisha bila wewe kujua limeishaje, basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi twende moja kwa moja kwenye hatua hizi.

Advertisement

Kwa kuanza moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kupakua app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload app hiyo moja kwa moja install na endelea kwa kufuata hatua hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload, moja kwa moja install app hiyo kwenye simu yako. Baada ya kuinstall fungua app hiyo na utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kubofya Get Started.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kuruhusu permission kwenye app hiyo, ruhusu permission kwa kubofya Next kisha Allow. Hikikisha una Allow kwani ni muhimu ili app hii iweze kufanya kazi vizuri.

Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa nyumbani, kwa kuwa mimi tayari nimesha tumia app hii utaweza kuona screen ya tofauti na iliyopo kwenye picha hapo chini. Kitu cha muhimu bofya ya ngao iliyo chini upande wa kushoto baada ya kitufe cha home.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Baada ya kubofya hapo sasa unatakiwa kuwasha firewall, bofya kitufe kikubwa kilichopo juu ya ukurasa huo. Baada ya kubofya hapo utaona kitufe hicho kimebadilika na kuwa On.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Baada ya kubofya kitufe cha ON, chini kidogo upande wa kulia utaona vidoti vitatu, kama inavyo onyesha kwenye picha hapo chini.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Bofya hapo kisha bofya Block All, ambayo itatokea mara baada ya kubofya vidoti hivyo vitatu vilivyopo juu kidogo upande wa kulia.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Baada ya hapo utaona confimation imetokea kwa chini, moja kwa moja bofya kitufe cha Apply kuweza kuthibitisha mabadiliko unayo yataka.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Baada ya hapo utakuwa umemaliza hatua ya kwanza ambapo kwa kufanya hatua hizo utakuwa umezuia app zote kwenye simu yako kutumia Internet hata kama internet itakuwa ipo On au imewashwa. Sasa hatua ya pili ni kuruhusu internet kwa baadhi ya app ambazo unataka kutumia tu.

Moja kwa moja ukiwa kwenye ukurasa huo huo wa pili kutoka upande wa kushoto, wenye alama ya ngao, moja kwa moja bofya kitufe cha kutafuta (search) kilichopo juu upande wa kulia, bofya hapo kutafuta jina la app ambayo unataka kufungua internet kwenye app hiyo pekee.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Moja kwa moja bofya alama ya Stop nyekundu iliyopo upande wa kulia pembeni ya jina la app husika kisha malizia kwa kubofya Apply.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Hakikisha alama ya stop imebadilika na kuwa alama ya mviringo wa kijani, hii ikiwa ina maanisha kuwa Internet imewezeshwa kwenye app husika.

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

Kwa kufanya hatua hizi utakuwa na uhakika app uliyowasha Internet tu ndio inayotumia Internet kwani apps nyingine zimekuwa na mtindo wa kutumia Internet bila kutoa taarifa, hii ni pamoja na app ya Facebook, TikTok na app nyingine kama Aliexpress na Google Services ambazo zote hutumia kiwango kikubwa sana cha data bila hata wewe kujua.

Kwa kufanya hatua hizi na kuhakikishia utaweza kutunza data yako kwa asilimia 100, hadi sasa mimi natumia programu hii na imekuwa msaada mkubwa sana kutoka kutumia GB 10 kwa siku tatu hadi kutumia GB 10 kwa siku 7 na wakati mwingine najisahau hadi zinarudishwa.

Hivyo basi kwa kufuata hatua hizi utaweza kutunza bando lako kwa asilimia kubwa hivyo jaribu njia hii kisha njoo niambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use