WhatsApp Kusitishwa kwa Baadhi ya Simu za iPhone na Android

Angalia kama simu yako inatumia mfumo huu
WhatsApp Kusitishwa kwa Baadhi ya Simu za iPhone na Android WhatsApp Kusitishwa kwa Baadhi ya Simu za iPhone na Android

Kila mwaka whatsapp imekuwa na mtindo wa kutangaza baadhi ya simu ambazo hazitakuwa na uwezo wa kutumia programu yake kwa mwaka ujao, mwaka huu sio tofauti kwani WhatsApp tayari imetangaza kuwa programu yake haitoweza kufanya kazi kwenye baadhi ya simu za Android pamoja na iPhone.

Kwa mujibu wa tovuti ya WhatsApp, hadi kufikia tarehe 1 mwezi wa pili mwaka 2020, programu ya WhatsApp itakuwa inafanya kazi kwenye simu za iPhone zenye mfumo wa iOS kuanzia iOS 9 na kuendelea. Simu zote za Apple zenye kutumia mfumo wa iOS 8 na kushuka chini zote hazitokuwa na uwezo wa kutumia programu hiyo hadi kufika kipindi hicho.

Mbali na hayo, watumiaji wenye simu zenye mfumo wa iOS ambao umebadilishwa kwa namna yoyote yaani (jailbroken), nao pia hawatoweza kutumia programu ya WhatsApp kwa asilimia 100 kama hapo awali. WhatsApp imebainisha kuwa haizui simu za namna hiyo kutumia programu yake bali programu hiyo haitoweza kufanya kazi kwa asilimia 100 au kwa maneno mengine ni kwamba inaweza kufanya kazi au inaweza isifanye kazi.

Advertisement

Kwa watumiaji wa mfumo wa Android na mifumo mengine kama Window Phone, WhatsApp imebainisha kuwa hadi kufikia mwezi wa kumi na mbili mwaka huu 2019 WhatsApp itasitisha kabisa upatikanaji wa programu yake kwenye simu za Windows Phone na pia kwenye simu zenye mfumo wa Android 2.3 (Gingerbread) nazo hazitoweza kufanya kazi kufikia wakati kipindi hicho.

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa programu ya WhastApp wenye simu zenye mifumo hiyo basi ni wakati wa kufikiria kutafuta simu mpya sasa, unaweza kutafuta simu kupitia HAPA.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use