WhatsApp Yaleta Uwezo wa QR Code Kwenye WhatsApp Business

Sasa anza kuchati WhatsApp kwa urahisi kwa kuscan QR Code
WhatsApp Yaleta Uwezo wa QR Code Kwenye WhatsApp Business WhatsApp Yaleta Uwezo wa QR Code Kwenye WhatsApp Business

Programu maarufu ya WhatsApp Business hivi karibuni imefanyiwa mabadiliko mapya ambayo yanaongeza urahisi kwa wafanyabiashara wote wanaotumia programu hiyo.

Mabadiliko hayo ni pamoja na sehemu mpya ya QR Code ambayo itamsaidia mtumiaji kuweza kuanza kuchati na biashara yoyote kwa haraka na urahisi. Sehemu hiyo itakuwa msaada zaidi kwa biashara zile zenye ofisi ambazo wateja wanapenda kutembelea mara kwa mara.

Mtumiaji anaweza kutengeneza QR Code na kuiweka kwenye sehemu inayo onekana na wateja wake na mara wateja wanapotaka kupata huduma zaidi kupitia WhatsApp wanaweza kuscan QR Code hiyo na kuanza kuchat na biashara husika.

Advertisement

WhatsApp Yaleta Uwezo wa QR Code Kwenye WhatsApp Business

Kupitia WhatsApp Business, unaweza kutengeneza QR Code kwa kuingia kubofya vitufe vitatu juu upande wa kulia kisha chagua Business tools – mwisho wa ukurasa huo chagua – Short link alafu chagua – View QR Code.

WhatsApp Yaleta Uwezo wa QR Code Kwenye WhatsApp Business

Pia kama unataka kuscan QR Code ya biashara yoyote unaweza kupitia hatua hizo hizo za kubofya sehemu ya Business toolsShort linkView QR Code – alafu chagua sehemu ya – Scan Code.

Kwa wale ambao wanataka kuprint QR Code hiyo unaweza kubofya sehemu ya share code kisha moja kwa moja chagua printer ambayo imeunganishwa kwenye simu yako alafu utaweza ku-print QR Code hiyo kwa ajili ya kuweka kwenye eneo la biashara au ofisi yako.

Mbali ya hayo, WhatsApp pia imeleta uwezo mpya ambapo sasa utaweza kushare link ya catalog yako moja kwa moja kwenye mitandao mbalimbali. Mtumiaji yoyote mwenye programu ya WhatsApp ataweza kuangalia catalog yako moja kwa moja kwa kubofya link yako.

WhatsApp Yaleta Uwezo wa QR Code Kwenye WhatsApp Business

Link hiyo unaweza kupata kupitia sehemu ya Business toolsCatalog – kisha bofya alama ya link iliyopo juu upande wa kulia na moja kwa moja utaweza kuona link yako na utaweza ku-copy link au kushare link hiyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Hata hivyo ili kusudi mtu aweza kuona bidhaa zako kwenye catalog ni lazima awe na programu ya WhatsApp.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use