Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Wabunifu wa Tehema Afrika Kupewa Bilioni 22 na Alibaba

Vijana wa kiafrika kuanza kunufaika na kampuni ya Alibaba
Alibaba Alibaba

Wataalamu na wabunifu wa tehema wa africa hivi karibuni wataanza kunufaika na kampuni ya Alibaba, kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la mwananchi. Hata hivyo baada ya kukamilisha ziara yake nchini Kenya wiki iliyopita, bilionea Jack Ma ambae ndio mwanzilishi wa kampuni hiyo ametangaza kuanzisha mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wa Kiafrika.

Ma ambaye ni mwanzilishi na mwenyekiti wa Kampuni za Alibaba, alitangaza kutoa Dola 10 milioni za Marekani (zaidi ya Sh22 bilioni ) kwa mwaka kwa ajili ya mfuko aliouanzisha ujulikanao kama African Young Entrepreneurs Fund. “Nataka kuzisaidia biashara za mtandaoni,” alisema Ma ambaye ni mshauri wa Shirika la Dunia la Maendeleo na Biashara (UNCTAD) kuhusu ujasiriamali na biashara ndogo kwa vijana.

Advertisement

“Fedha zipo. Ni zangu, hivyo sina haja ya kuomba kibali cha yeyote kuzitumia,” alisisitiza akibainisha kwamba ataajiri watu wa kuzisimamia na mchakato huo uanze haraka mwaka huu. Ma alisema atashirikiana na UNCTAD kuwapata vijana 200 wabunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambao wataenda nchini mwake, kujifunza kutoka kwenye Kampuni ya Alibaba aliyoianzisha 1999 na sasa ina thamani ya Dola 231 bilioni za Marekani (zaidi ya Sh510 trilioni).

Hata hivyo Ma aliusema mpango huo alipokuwa kwenye ziara yake ya kwanza barani Afrika, Ma amezitembelea nchi za Kenya na Rwanda na mpango huo aliubainisha alipohudhuria mkutano wa Youth Connekt Africa, uliofanyika Jumatatu huko Kigali nchini Rwanda. Kiongozi huyo Pia, alibainisha nia yake ya kushirikiana na vyuo vikuu vya Afrika kufundisha teknolojia ya intaneti, uundaji wa roboti na biashara ya mtandaoni.

Ma pia alisema kuwa alisikitishwa na kukosekana kwa intaneti kwenye baadhi ya maeneo akisema huduma hiyo ni muhimu kuliko ilivyokuwa umeme zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Mwananchi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use