Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mwanzilishi wa Amazon Sasa Ndie Tajiri Mkubwa Zaidi Duniani

Jeff Bezos amempiku Bill Gates kuwa mtu tajiri zaidi Duniani
Kampuni ya Amazon Kampuni ya Amazon

Mmiliki namuanzishaji wa kampuni ya Amazon ambae anajulikana kwa jina la jeff bezos sasa ndio anasemekana kuwa mtu tajiri zaidi duniani. Mtandao wa bbc swahili umeandika kuwa Jeff amekuwa tajiri akiwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 90.6.

Hata hivyo tovuti ya bbc imendelea kuandika kuwa, ongezeko la hisa za Amazon siku ya Alhamisi lina maanisha kwamba thamani ya bwana Jeff imeishinda ile ya mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates bwana jeff kwa sasa anamiliki mara tano ya hisa hizo ambazo thamani yake imepita dola bilioni 500.

Advertisement

Katika miaka ya hivi karibuni jeff, aliangazia biashara yake ya roketi ya angani ya Blue Origin pamoja na gazeti la Washiington Post, ambalo anamiliki. Vilevile vifaa vya kiteknolojia vimeongeza ukuwaji wa thamani za biashara kwa muazilishi hiyo wa kampuni ya Amazon.

Katika kujua baadhi ya utajiri wa mwanzilishi huyo, gazeti la Washington post liliandika kuwa Mapema mwaka huu bwana jeff alilipa dola milioni 23 kununua eneo la kumbukumbu la kiwanda cha nguo cha zamani mjini Washington DC, Kiwanda hicho Kitakapo badilishwa kitakuwa nyumba ya familia ya jeff ambayo itakuwa majirani wa Obama pamoja na Ivanka Trump na Mumewe Jared Kushner.

Jeff Bezos pia anamiliki gazeti hilo la Washington post ambalo alilinunua kwa dollar za marekani milioni 250 fedha zake taslimu, jeff pia ana nyumba katika mji wa Seattle na Beverly Hills miji ambayo inasifika kukaa watu matajiri na mastaa wa muziki na filamu wa marekani.

UPDATE : Bill Gates Harudi Kuwa Tajiri wa Dunia Boss Jeff Bezos alimpiku kwa muda mchache Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani siku ya Alhamisi kufuatia kupanda kwa hisa za mfanyibiashara huyo kabla ya ripoti ya mapato yake ya hisa kushuka tena. – BBC Swahili

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : BBC

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use