Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Google Kutoa Mafunzo Kwa Watu Milioni 10 Afrika

Google kujitolea mafunzo wa watu zaidi ya Milioni 10 barani Afrika
Google Afrika Google Afrika
PICHA GOOGLE AFRICA BLOG

Google ni moja kati ya kampuni kubwa na bora za teknolojia duniani, kampuni hii inajulikana kwa kuwa na baadhi ya bidhaa kama vile mfumo wa uendeshaji wa Android, Simu ya Google Pixel pamoja na bidhaa nyingine nyingi.

Katika kuongeza matumizi ya mtandao pamoja na ujuzi wa kutumia mtandao, kampuni ya Google ina mipango ya kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika kuhusu njia za kutumia mitandao katika kipindi cha miaka mitano inayokuja kwa lengo la kuwawezesha kupata ajira.

Advertisement

Msemaji wa kampuni hiyo anasema kuwa, Google pia itawapa mafunzo wahandisi wa mitandoni 100,000 nchini Nigeria, Kenya na Afrika Kusini. Hata hivyo hadi kufikia mwezi Machi Google ilisema kuwa tayari ilikuwa imefikia lengo lake la kuwapa mafunzo watu zaidi ya milioni moja.

Mkurugenzi wa Google Sundar Pichai amesema kuwa kampuni hiyo imejitolea kuwandaa watu wengine milioni 10 kwa ajira siku za usoni katika kipindi cha miaka mitano inayokuja. Kulingana na Google blog mafunzo hayo yanayotolewa kwa lugha kadha zikiwemo Kiswahili, Hausa na Zulu, na yatahakikisha kuwa asilimia 40 ya watu ambao watapewa mafunzo hayo ni wanawake.

Bara la Africa sasa lipo kwenye wakati mzuri sana kwa upande wa teknolojia, hivi juzi mwenyekiti wa makampuni ya Alibaba pia alitoa ahadi inayo fanana na hii ya kuwasaidia wataalamu wa tehema barani Afrika kwa kuwapa zaidi ya bilioni 22 za kusadia kampuni changa zinazo chipukia kutoka Afrika, ikiwa ni pamoja na kusaidia vijana wa kiafrika zaidi ya 200 kwenda nchini china kujifunza kupitia makampuni ya Alibaba. Fursa ndio hizi…..

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : BBC Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use