Malware Virus Zagundulika Kwenye Kompyuta za Macbook

Hii Ndio Aina mpya Malware iliyogunduliwa hivi karibuni kwenye kompyuta za Macbook
Mac Malware Mac Malware

Kampuni maarufu ya Apple Inc huenda ndio kampuni yenye wataalamu wakubwa wa ulinzi pamoja na uwezo mkubwa wa kulinda vifaa vyake mbalimbali kama vile iPhone pamoja na Macbooks. Hata hivyo sio kwamba vifaa hivi vinaulinzi asilimia 100 hapana ! hii inatokana na kwamba ningumu sana kwa vifaa vya electronics kuaminika asilimia 100.

Hivi karibuni kumegunduliwa aina mpya ya malware kwenye kompyuta zinazoaminika kuwa hazingii virus yaani hapa nazingumzi kompyuta za Macbook, Malware hizo zimegunduliwa na wataalamu kutoka katika kampuni ya Malwarebytes Corporation kampuni iliyotengeneza programu ya kuzuia malware kwenye kompyuta za mac yaani (Malwarebytes Anti-Malware software).

Malware hizi zinauwezo wa kufungua baadhi ya tovuti ambazo zinakufanya uweze kupakua programu zisizo na maana kwenye kompyuta yako ya Mac, hata hivyo kiongozi wa kampuni ya Malwarebytes Thomas Reed, alieleza kuwa Malware hizi zimepatikana kwenye tovuti official ya Advanced Mac Cleaner ambapo uwezo malware hizo unategemeana sana na uwezo wa mtumiaji kutoku gundua scam au utapeli kwenye tovuti hiyo.

Advertisement

Malware hizi huingia kwenye kompyuta yako ya mac pale mtumiaji anapokubali kuinstall programu ya Advance Mac Cleaner kwa kuinstall programu hiyo programu nyingine ya Mac File Opener huwa installed sambamba na programu hiyo ya Advance Mac Cleaner, Mr Reed aliongeza kwa kusema ilikuwa ni ngumu sana kugundua programu hiyo kwa mara ya kwanza kwani programu hiyo ilionekana kukaa tu kwenye folder zake na pia haikuonekana kwenye mafaili ya log-in items.

Wakiendelea kuchunguza zaidi kwenye programu hiyo wataalamu hao waligundua file linaloitwa Info.plist file hilo lilionyesha kuwa na uwezo wa kufungua mafile mengine 232 yenye format tofauti tofauti hivyo pale mtumiaji anapofungua file hilo programu ya Mac File Opener hufunguka na kuonyesha aina feki ya programu pamoja na version ya programu hiyo zote hutokea kwenye box maarufu kama authentic OS X dialog box likiwa na maelezo ya kuwa programu yenye mafaili hayo haijawa installed kwenye kompyuta yako ya Mac. Hata hiyo box hilo hukupeleka moja kwa moja kwenye tovuti ya macfileopener.com hapo programu za PCVARK zitapakuliwa moja kwa moja kwenye kompyuta yako programu hizo ni kama vile Mac Space Reviver pamoja na Mac Adware Remover, chakushangaza hapa ni kwamba programu zote hizi zina developer certificate ambazo hutolewa na Apple wenyewe, hii husababisha programu hizi kuinstall kwenye kompyuta yako bila taarifa yoyote ya kukutaadharisha.

Hivyo kama wewe ni mtumiji wa kompyuta za Mac tafadhali kuwa makini sana na kompyuta yako na install progarmu kutoka kwenye App Store peke yake kwani Virus hizi ni mbaya sana na Husumbua sana zinapoingia kwenye kompyuta yako.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia App yetu ya Tanzania Tech App au kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya  facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use