Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Ndio Laptop Bora za Kununua Ndani ya Mwezi Huu

Hizi ndio laptop nyingine 15 bora ambazo unaweza kununua ndani ya mwaka 2016 pamoja na bei zake kwa dollar na Tsh
Laptop Bora Laptop Bora

Kama umekua mfuatiliaji wa tovuti ya tanzania tech na uhakika utakua umesha soma makala inayosema laptop bora za kununua mwaka 2016, kwenye makala hiyo tulijadili baadhi ya laptop bora mabazo zilikua zikifanya vizuri kwa muda huo. Lakini sasa makala hii ya leo tutaenda kuangalia laptop 15 bora ambazo unaweza kununua hivi sasa, bila shaka tutakua wote mpaka mwisho wa makala hii tukizihesabu na kuchambua laptop hizo bora 15..Okay let’s goo.

Dell XPS 13

Advertisement

dell

Sifa za Dell XPS 13

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 520 – Intel Iris Graphics 540
  • RAM: 4GB – 8GB
  • Screen: 13.3-inch FH (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800)
  • Storage: 128GB – 256GB SSD

Dell XPS 13 ni moja kati ya laptop bora sana laptop hii imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana pamoja kuwa na uwezo mkubwa wa kukaa na chaji. Laptop hii ina kioo chembamba sana pamoja na processor mpya yenye nguvu ya Intel’s Skylake, hakika hii ndio laptop bora sana ambayo unaweze kununua sasa hivi.

$850.00 = TSH 1,854,437.56

NUNUA AMAZON

Asus ZenBook UX305

asus-zenbook-ux305

Sifa za Asus ZenBook UX305

  • CPU: Intel Core M3-6Y30 – M7-6Y75
  • Graphics: Intel HD Graphics 515
  • RAM: 8GB
  • Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3200 x 1800) IPS display
  • Storage: 256GB – 512GB SSD

Asus ZenBook UX305 ni moja kati ya laptop bora ambazo zimefanana sana na Macbook basi kama wewe unatafuta laptop ambayo ina muundo mzuri pamoja na nguvu zaidi laptop hii ni bora sana, pia Asus ZenBook UX305 inakaa na chaji kwa muda wa karibia masaa 72 hivyo kama unatafuta jembe la kazi pamoja na muonekano Asus ZenBook UX305 ni kwaajili yako.

$693.66 = TSH 1,513,351.95

NUNUA AMAZON

Toshiba Chromebook 2

toshiba-chromebook-2

Sifa za Toshiba Chromebook 2

  • CPU: Intel Celeron – Core i3-5015U
  • Graphics: Intel HD Graphics – HD Graphics 5500
  • RAM: 4GB
  • Screen: 13.3-inch, 1,920 x 1,090
  • Storage: 16GB eMMC

Toshiba Chromebook 2 ni laptop bora kama unatafuta laptop yenye kioo angavu pamoja na nguvu ya kufanya karibia kazi yoyote. Toshiba Chromebook 2 inkuja na mfumo bora wa uendeshaji wa Chrome OS hii ikiwa inakupa uwezo wa kuinstall baadhi ya programu za Android kwenye laptop yako, kwa upande wa chaji laptop hii inakaa na chaji kutokana na matumizi yako hivyo kama unajua unataka kuitumi kwa muda mrefu ni vizuri kukumbuk kubeba chaji.

$209.99 = TSH 459,074.81

NUNUA AMAZON

 MacBook Air inch-13

13-inch-macbook-air

Sifa za MacBook Air inch-13

  • CPU: Intel Core i5
  • Graphics: Intel HD Graphics 6000
  • RAM: 8GB
  • Screen: 13.3-inch, LED-backlit glossy display (1,440 x 900)
  • Storage: 128GB – 256GB SSD

Kama unatafuta laptop ngumu yenye uwezo mkubwa basi MacBook Air inch-13 ni laptop bora kuwa nayo, laptop hii ni nyepesi lakini wepesi wake sio sawa na uwezo wake kwani laptop hii inauwezo mkubwa wa kufanya karibia kila kazi lakini kama ni graphics designer ninge-kushauri kuangalia laptop nyingine kwenye list hii. Kwa upande wa chaji laptop hii inauwezo wa kukaa na chaji masaa 13 hivyo kumbuka kubeba chaja (charger) pale unapotaka kutumia laptop hii siku nzima.

$859.00 = TSH 1,877,924.01

NUNUA AMAZON

Samsung Notebook 9

samsung-notebook-9

Sifa za Samsung Notebook 9

  • CPU: 2.3GHz Intel Core i5-6200U
  • Graphics: Intel HD Graphics 520
  • RAM: 8GB
  • Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) LED anti-reflective display
  • Storage: 256GB

Kama unatafuta laptop bora yenye kudumu na chaji na yenye kioo bora Samsung Notebook 9 ni laptop bora kwaajili yako. Laptop hii ni bora kuliko Macbook Air kwani laptop hii inatumia processor mpya ya Core i5 Skylake hili pekee linafanya laptop hii kuwa bora zaidi, pia kwa chaji laptop hii iko vizuri sana huvyo kama unatafuta laptop bora yenye kudumu na chaji na yenye kioo bora Samsung Notebook 9 ndio laptop ya kununua.

$899.00 = TSH 1,965,370.99

NUNUA AMAZON

Surface Book

surface-book

Sifa za Surface Book

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel HD graphics 520 – Nvidia GeForce graphics
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.5-inch, 3,000 x 2,000 PixelSense Display
  • Storage: 128GB – 256GB PCIe3.0 SSD

Kama unatafuta laptop bora yenye kutumia window 10 basi hii ni laptop bora ambayo sasa hivi unaweza kununua. Laptop hii inauwezo mzuri sana kwa wale wanaopenda laptop zinazotumia windows na ni moja kati ya laptop yenye nguvu na uwezo mzuri sana, kuhusu chaji laptop hii inakaa na chaji wastani..soo kumbuka kubeba chaja unapotaka kutumia laptop hii siku nzima.

$1332.68 = TSH 2,913,471.21

NUNUA AMAZON

HP Spectre

hp-spectre

Sifa za HP Spectre

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 520
  • RAM: 8GB LPDDR3 SDRAM
  • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) IPS UWVA WLED
  • Storage: 256GB – 512GB SSD

Unapoina laptop ya HP Spectre kwa mara ya kwanza unaweza kudhani laptop hii itakuwa ni bei ghali sana, lakini kwa uonekano bora pamoja na uwezo mkubwa HP Spectre ni laptop yenye uwezo mkubwa kuliko hata laptop mpya ya sasa ya Macbook, laptop hii inauwezo wa hali ya juu pamoja na battery yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa kiwango kikubwa sana.

$00 = TSH 00

NUNUA AMAZON

Samsung Notebook 7 Spin

samsung-notebook-7-spin

Sifa za Samsung Notebook 7 Spin

  • CPU: 2.5GHz Intel Core i7-6500U
  • Graphics: Nvidia GeForce 940MX (2GB DDR3L); Intel HD Graphics 520
  • RAM: 12GB – 16GB
  • Screen: 15.6-inch Full HD (1,920 x 1,080) LED with touch panel
  • Storage: 1 TB HDD – 1TB HDD; 128GB SSD

Kama ulisha wahi kutamani kuwa na Macbook Pro kwa bei rahisi basi Samsung Notebook 7 Spin inakupa muonekano pamoja na nguvu kama ya Macbook Pro. Samsung wamesogea mbele zaidi kwa kuweka kwa kuongeza Touchscreen kwenye laptop hi bora na ya kijanja. Zaidi ni kwamba laptop hii inatumia teknolojia ya kioo cha HDR ambayo kwa sasa bado haiko kwenye kompyuta nyingi, kuhusu battery Samsung Notebook 7 Spin ni kama vile Power Bank kwani laptop hii inauwezo mkubwa sana wa kukaa na chaji.

$664.80 = TSH 1,453,368.90

NUNUA AMAZON

HP Spectre x360

hp-spectre-x360

Sifa za HP Spectre x360

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 620
  • RAM: 4GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – UHD (3,840 x 2,160) IPS UWVA-backlit multi-touch
  • Storage: 128GB – 512GB SSD

Kama unapenda laptop zenye touchscreen zenye uwezo mkubwa basi HP Spectre x360 ni laptop bora sana kwako, kwani inakupa uwezo wa kutumia laptop yako jinsi unavyotaka kuanzia kwenye uwezo wa laptop yenyewe mpaka kwenye muonekano. Laptop hii inao uwezo wa kukaa na chaji kwa masaa 8 mpaka 9 zaidi ni kwamba laptop hii imeongezewa uwezo wa kujaa chaji haraka sana, kwa hiyo kama wewe ni mtu ambao uko bize na unapenda touchscreen laptop hii ni bora sana kwaajili yako.

$550.98 = TSH 1,204,538.50

NUNUA AMAZON

MacBook (2016)

macbook-2016

Sifa za MacBook (2016)

  • CPU: Intel Core m3 – m5
  • Graphics: Intel HD Graphics 515
  • RAM: 8GB
  • Screen: 12-inch, 2304 x 1,440 LED-backlit IPS display
  • Storage: 256GB – 512GB SSD

Kama wewe ni team Apple basi MacBook ya Mwaka 2016 ni chaguo bora sana kwako, kuiacha kuwa laptop za Apple ni Legends kwa kuwa na muundo bora, toleo la mwaka huu ndilo bora sana kwani Apple iliamua kuweka rangi ya Rose Gold kwenye Laptop hii bora kwa style na muonekano. Vilevile kama unatafuta laptop ya kazi MacBook ya 2016 ni laptop yako kwani inauwezo wa kufanya karibia kila kazi, kwa upande wa chaji well..we all know don’t we..? laptop hii inauwezo wa kukaa na chaji kwa kiasi flani hivyo kumbuka chaja yako kama unatoka kwenda safari ya mbali na laptop yako.

$1199.99 = TSH 2,623,387.70

NUNUA AMAZON

Lenovo Yoga 900

lenovo-yoga-900

Sifa za Lenovo Yoga 900

  • CPU: 2.5GHz Intel Core i7-6560U
  • Graphics: Intel Iris Graphics 540
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch QHD+ 3,200 x 1,800 IPS display
  • Storage: 512GB – 1TB SSD

Kama unatafuta laptop ya kisasa yenye muonekano bora na nguvu ya hali ya juu Lenovo Yoga 900 ni laptop bora sana kwaajili yako. Laptop hii inauwezo wa hali ya juu wa kuonyesha picha angavu pamoja na kuwa na speed ya hali ya juu sana kwa upande wa storage lapto hii pia imeonekana kuwa na uwezo wa kuwa na storage kubwa wakati mwingine mpaka 2TB. Kuhusu chaji laptop hii iko vizuri kwenye upande wa chaji lakini kama unaitumia sana dont forget your charger.

$1136.91 = TSH 2,485,483.80

NUNUA AMAZON

MacBook Pro 13-inch yenye Retina display

macbook-pro-13-inch

Sifa za MacBook Pro 13-inch yenye Retina display

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel Iris Graphics 6100
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch IPS, 2,560 x 1,600 pixels
  • Storage: 128GB – 512GB SSD

MacBook Pro 13-inch yenye Retina display ni laptop ambayo ni bora kwa matumizi karibia ya kila mtu iwe wewe ni mwanafunzi, graphic designer, photographer, DJ au hata mtu mwingine yoyote MacBook Pro 13-inch yenye Retina display ni laptop bora sana kwako. Wote tunajua uwezo wa laptop hii ukweli ni kwamba laptop hii ni moja kati ya laptop bora sana kukunua siku hizi. Kuhusu chaji lapto hii inauwezo mzuri sana wa kukaa na chaji hivyo shaka ondoa unapowaza kununua MacBook Pro 13-inch yenye Retina display.

$1199.00 = TSH 2,621,223.38

NUNUA AMAZON

HP Spectre x2

hp-spectre-x2

Sifa za HP Spectre x2

  • CPU: Intel Core m5 – m7
  • Graphics: Intel HD Graphics 515
  • RAM: 8GB
  • Screen: 12-inch, 1,920 x 1,280 WUXGA+ IPS WLED-backlit touchscreen
  • Storage: 128GB – 512GB SSD

Kama unatafuta kompyuta yenye muonekano bora pamoja na nguvu kubwa kwa kazi za kawaida HP Spectre x2 ni Laptop bora kwajili yako. Kama unatafuta laptop ambayo ni nyepesi na ambayo inauwezo wa kukuruhusu kufanya kazi zako za kawaida basi laptop hii ni bora sana kama unataka kuinunua ndani ya mwaka huu 2016. Kuhusu battery laptop hii inajiweza kiasi kutokana na matumizi yako hivyo kumbuka unapoitumia sana usisahau kubeba chaja.

$474.93 = TSH 1,038,279.92

NUNUA AMAZON

HP Chromebook 14

hp-chromebook-14

Sifa za HP Chromebook 14

  • CPU: 1.83GHz Intel Celeron N2940 processor
  • Graphics: Intel HD Graphics
  • RAM: 4GB DDR3
  • Screen: 14-inch 1,920 x 1,080 display
  • Storage: 16GB eMMC

Kama unatafuta kompyuta itakayo kupa test ya mfumo wa uendeshaji kutok Google yani Chrome OS basi HP Chromebook 14 ni kwaajili yako. Komputer hii inauwezo wa kawaida wa kufanya kazi za kawaida na pia kama ni mpenzi wa game za android laptop hii ni bora sana. Kingine bei ya laptop hii ni nzuri sana hivyo ni rahisi kuipata na kuitumia pia, kuhusu battery well kama matumizi yako ni makubwa usisahau kubeba chaji kwenye mkoba wako.

$169.99 = TSH 371,627.83

NUNUA AMAZON

Lenovo ThinkPad X1 Yoga

lenovo-thinkpad-x1-yoga

Sifa za Lenovo ThinkPad X1 Yoga

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 520
  • RAM: 8GB
  • Screen: 14-inch, FHD (1,920 x 1,080) – WQHD (2560 x 1440) IPS touchscreen
  • Storage: 180GB – 512GB NVMe SSD

Kama unatafuta laptop bora yenye muonekano wa kisasa pamoja na uwezo wa hali yajuu Lenovo ThinkPad X1 Yoga ni laptop bora sana kwako. Laptop hii ni nzuri kwa matumizi ya kila mtu isipokua laptop hii haidumu na chaji kabisa kwani laptop hii inaonekana kukaa na chaji kwa masaa 3 na dakika 29, hivyo kama haujali swala la kutembea na chaji yako kwenye mkoba basi laptop hii ni bora sana kununua kwa mwaka huu 2016.

$674.36 = TSH 1,474,268.72

NUNUA AMAZON

Je unasemaje husu laptop hizi kama kama una maoni tuandikie hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

4 comments
  1. Mnauzaje Laptop ndogo size 11.6 au chini(netbook) ambazo ni touch screen, Os yake ni windows, RAM 4GB au zaidi, HDD 500 GB, USB ports 3 (mojawapo ni USB 3.0), HDMI, VGA, resolution 1024 x 768 au zaidi, WIFI, bluetooth, SD card reader.

    Naitwa Lawi Mshana
    mshanalawi@gmail.com

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use