Dell Yaweka Processor ya Kaby Lake kwenye Laptop yake ya XPS 13

Dell wamerudi kivingine tena baada ya kuweka processor ya Kaby Lake kwenye laptop yake ijulikanayo kama XPS 13
laptop-dell-xps-13-3 laptop-dell-xps-13-3

Kampuni maarufu ya utengenezaji wa kompyuta ya Dell hivi karibuni imetangaza kurudisha kompyuta yake ya XPS 13 sokoni ikiwa na muonekano mpya kabisa kuanzia rangi mpaka uwezo wa kompyuta kwa ujumla.

Kampuni hiyo imetangaza kurudisha laptop yake hiyo ikiwa na processor mpya na ya kisasa kutoka katika kampuni ya intel yani intel kaby lake, hii ni moja kati ya processor zenye nguvu zaidi ya zile za intel core i7 ambazo ndio zinapatikana sana kwenye kompyuta za Apple maarufu kama Macbooks.

Akielezea mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alisema Dell imepanga kuwaridhisha wateja wake kwa kuweka rangi mpya na maarufu ya Rose Gold kwenye laptop hii ambayo kuanzia itoke mwaka 2015 mpaka sasa haijapoteza ubora wake kwani sifa na muundo wa laptop hii ni wa kisasa kila siku, alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya Dell ya nchini Marekani.

Advertisement

Maboresho mengine yanayokuja kwenye laptop hiyo ni pamoja na battery inayokaa zaidi ya masaa 22 kwa laptop hiyo yenye kioo cha 1080p na masaa 13 kwa laptop yenye kioo cha 4K pia laptop zote hizi zitakuja na kioo cha inch 13, pia kampuni hiyo inasema kuwa imebadilisha laptop hiyo kuwa ya aluminum pamoja na carbon fiber ili kufanya laptop hiyo idumu zaidi vilevile kwa upande wa kioo laptop hiyo itatumia teknolojia ya Gorilla Glass ili kulinda kioo cha laptop hiyo dhidi ya michubuko.

Pia kwa upande wa RAM kompyuta hiyo inatarajiwa kuja na RAM ya 8GB ikiwa na uwezo wa kusonga mpaka 16GB pamoja na Hard Disk ya 1TB, pia Graphics ya XPS 13 itakuja na Intel’s HD Graphics 650 ambayo itakupa uwezo wa kawaida wa kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kucheza Game zenye uwezo mkubwa.

Bei ya laptop hii kwa marekani itauzwa dollar za kimarekani  $799 sawa na shilingi ya kitanzania Tsh 1,752326.85 na ile yenye rangi ya Rose Gold itauzwa dollar za kimarekani $1,499 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 3,287531.85 bei zote hizo za tanzania ni kwa viwango vya kubalidili fedha vya tarehe 19-09-2016.

Laptop hizo zimepangwa kupatikana kuanzia tarehe 4 mwezi october mwaka huu, ili kujua zaidi kuhusu laptop hii pamoja na siku itakapo fika Tanzania endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use