Safaricom Kuruhusu Kutuma Pesa Kati ya MPesa na Paypal

Sasa wateja wa M-Pesa wataweza kupokea na kutuma pesa kupitia PayPal
Mpesa Mpesa

Hivi karibuni wananchi wa nchini Kenya wataanza kunufaika kutokana na ushirikiano mpya kati ya kampuni ya huduma za Simu ya Safaricom na kampuni ya kupokea malipo ya mtandaoni ya PayPal, ushirikiano huo unalenga kuwezesha wananchi wa nchini humo kuweza kutuma na kupokea pesa kutoka huduma ya Safaricom ya M-Pesa kwenda PayPal na Paypal kuja kwenye Wallet ya M-Pesa.

Aidha, ushirikiano huo utawawezesha wafanya biashara za mtandaoni nchini humo kuweza kupokea malipo mtandaoni kwa urahisi kwa kutumia huduma hiyo. Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa Atlas, M-pesa kwa nchini Kenya ni moja kati ya huduma zinazo tumiwa sana ukilinganisha na huduma zingine zinazofanana na M-pesa.

Hata hivyo hatua ya kuja kwa ushirikiano huu inakuja wakati ni miezi michache kutoka kampuni ya Safaricom ya nchini Kenya, kuzindua soko lake la mtandaoni maarufu kama Masoko, ambalo linawawezesha wateja wa mtandao huo wanao tumia huduma za M-pesa kuweza kununua bidhaa na kufanya malipo kwa kutumia huduma ya M-Pesa.

Advertisement

Safaricom imekua na juhudi za ziada kuendeleza huduma za mtandaoni, kwani hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza kuwa inategemea kuanza ushirikiano na kampuni ya Google ili kuwaruhusu wateja wake wa M-pesa kuweza kununua au kufanya malipo ya programu au Apps mbalimbali kupitia soko la Google Play Store kwa kutumia huduma za malipo za M-Pesa.

Kwa sababu Safaricom ni kama Kampuni ya Vodacom kwa hapa Tanzania, labda tutegemee ujio wa huduma hizi nzuri kwa hapa Tanzania kwa siku za karibuni ukizingatia mwenyekiti mtendaji mpya Sylivia Mulinge, atakaye kuja kuongoza Vodacom Tanzania anatokea kampuni ya Safaricom ya nchini Kenya.

2 comments
  1. Daafadhali tupatehuduma hii na sisi.. Mkenya atatusaidia hakika maana tz tunahitajipaypalna mpesa connect2

  2. kwa tanzania tunaweza kutuma pesa kwenda kenya kwa kutumia vodacom mpesa na mtu akapata pesa hiyo vizuri kwa kutumia safaricom mpesa je? kwa alieko kenya sasa anaweza kutuma pesa kwa safaricom na ikanifikia kwenye mpesa ya vodacom tanzani msaada plz………

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use