Hatua za Kufuata Kuweza Kufanya Manunuzi Mtandaoni

Unataka kuweza kufanya manunuzi mtandaoni..? Fuata hatua hizi
Kufanya manunuzi mtandaoni Kufanya manunuzi mtandaoni

Ni kweli kumekuwa na tatizo kubwa hasa hapa Tanzania kwenye njia za kufanya manunuzi mtandaoni, matatizo haya yanasababishwa na kukosekana kwa njia rahisi za malipo ambazo zinawezesha watanzania wote bila kujali kipato kuweza kufanya manunuzi mtandaoni.

Ni kweli kwamba hapa kwetu Tanzania teknolojia bado iko nyuma kidogo ukilinganisha na nchi jirani kama ilivyo Kenya na nchi nyingine. Hivi karibuni tulisikia majirani zetu wakiwezeshewa huduma ya malipo ya mtandaoni ya Paypal kupitia huduma za Malipo ya simu za M-pesa ambapo watumiaji wa huduma za M-pesa wataweza kutuma pesa kati ya PayPal kuja M-Pesa na M-Pesa kuja Paypal.

Lakini kwa hapa Tanzania huduma hii bado haijawezeshwa lakini pia ni wazi watu wengi hapa nchini Tanzania wangependelea kuweza kufanya manunuzi mtandao, ndio maana leo Tanzania Tech tunakuletea hatua za kufuata ili kuwezesha kupata kadi ya benki yenye kuweza kufanya manunuzi mtandao, basi bila kupoteza muda twende tuka jifunze hatua hizo za muhimu.

Advertisement

  • Fungua Akaunti ya Benki (Haina Haja ya Kuwa na Hela Nyingi)

Hatua ya kwanza ili uweze kufanya manunuzi mtandaoni ni pamoja na kuhakikisha unapata kadi ya benki, kadi hiyo ya benki inatakiwa iwe na uwezo wa MasterCard au Visa pia ni lazima iwe imeunganishwa na huduma ya kufanya manunuzi mtandaoni. Hivyo basi unachotakiwa kufanya ni kwenda benki yoyote ambayo unataka kisha fungua akaunti ya kawaida, gharama za kufungua akaunti huwa ni bure lakini ni lazima uwe na kiwango cha kuanzia kuweka kwenye akaunti yako, unaweza kuweka kuanzia Tsh 20,000 na kuendelea inategemeana na benki.

  • Omba Kadi ya ATM yenye Uwezo wa MasterCard au Visa

Baada ya kufungua akaunti yako, hatua inayofuata ni kuomba kadi ya ATM yenye Visa au MasterCard gharama zake pia hizi hutegemeana na benki hiyo ni vizuri kuomba utaratibu ili kuja inachangiwa gharama kiasi gani, pia usisahau kwenda na picha na vitambulisho vyako.

Baada ya kuomba kadi ya ATM yenye huduma za Visa au MasterCard hatua inayofuata baada ya kupata kadi yako ni kuomba huduma za kufanya manunuzi mtandaoni, Huduma hizi hutolewa kama huduma za ziada na pia sio kila kadi inayokuja inakuja na huduma hizi tayari hivyo ni lazima kuziomba huduma hizi kupitia benki yako na benki yako ndio itawezesha huduma hizo kwenye kadi yako na hapo unatakiwa kujaza fomu nyingine yenye data binafsi za muhimu na sahihi yako.

Mara baada ya kupata huduma zote hizo sasa unaweza kuendelea kwenye hatua inayofuata. Kumbuka hatua zote hizo zinaweza kuchukua muda kuanzia wiki mbili au zaidi kutokana na muda wa kutengeneza ATM pamoja na muda wa kuwezeshwa na huduma za manunuzi ya mtandaoni.

  • Wezesha Huduma ya Manunuzi Mtandaoni (Paypal au Zingine)

Baada ya kufanya hatua hizo zote sasa unaweza kufanya manunuzi mtandaoni kwa kuwezesha huduma mbalimbali kama PayPal na nyingine. Kumbuka inakuhitaji kuweka pesa kwenye akaunti yako kabla ya kufanya manunuzi mtandaoni pia inakuhitaji kujua viwango vya kubadilisha fedha ili kuweza kujua ni kiasi gani unachotakiwa kuweka kwenye akaunti yako.

Kama unataka kujiunga na huduma za PayPal unaweza kusoma hapa pia unaweza kuangalia video hapo chini yenye hatua zote jinsi ya kujiunga na PayPal tayari kufanya manunuzi kwenye tovuti maarufu kama ebay, Amazon na nyingine nyingi.

Baada ya kufuata hatua zote hizo na imani utakuwa umeweza kufanya manunuzi mtandaoni. Kama una swali au kama una mahali ambapo umekwama unaweza kuuliza swali lako pitia maoni hapo chini au unaweza kujiunga na akaunti yetu ya Telegram Tanzania Tech kwaajili ya kupata msaada wa karibu zaidi.

3 comments
  1. kwanza pole na kazi naomba msaad jinsi ya kununua vitabu kwenye mtandao hasa vile vilivyoandikwa kwa kiswahili na vyaaudio pia kama inawezekana

  2. nawapenda Sana na nimewaelewa Sana Sana Mungu azid kuwapa akil nying ila nna deal lingne kuhus manunuz mtandaon nimeskia Kuna mpesa master card na Airtel master card ambazo pia zinawezesha kufanya manunuz mtandaon je izo zipoje Kama zipo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use