Jinsi ya Kupokea Pesa Mtandaoni Kutoka Nje ya Tanzania

Njia za kuwezesha kupokea pesa Mtandaoni kutoka nje ya Tanzania
Kupokea pesa mtandaoni Kupokea pesa mtandaoni

Pamoja na kukuwa kwa teknolojia na kuongezeka kwa watu wengi wanaofanya biashara mtandaoni, lakini bado njia za kupokea pesa mtandaoni kutoka nje ya nchi kuja ndani ya nchi ni chache sana hasa hapa nchini Tanzania. Mbali na hayo, njia nyingine ambazo zinajulikana kuwezesha kupokea pesa mtandaoni hutoza gharama kubwa sana na pia kutumia muda mrefu sana pesa kumfikia muhusika.

Ndio maana leo Tanzania Tech tunakuletea njia za kuweza kukusaidia kupokea pesa mtandaoni kutoka nje ya Tanzania. Njia hizi zinatumika na watu mbalimbali na zipo kwa muda mrefu hivyo niwazi kuwa ni salama na za uhakika. Baadhi ya njia hizi tayari mimi binafsi nimesha zitumia hivyo nitakuambia yote ya muhimu unayotakiwa kujua ili kuwezesha huduma hizo, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hizi.

  • Payoneer

Payoneer ni moja kati ya huduma za muda mrefu sana za kupokea pesa mtandaoni na ni moja kati ya huduma inayotumiwa na watu wengi wanaopendelea kupokea malipo kwa njia ya mtandao kutoka nje ya nchi kuja nchini Tanzania. Huduma hii ni moja ya huduma ambayo binafsi nimesha itumia na kiukweli nimefurahishwa sana na huduma zao hasa pale ninapotaka kupokea pesa kutoka kwa makampuni makubwa ya nje ya nchi, kama Amazon.

Advertisement

Njia hii haikuitaji kwenda benki ili kuwa na huduma hii, bali unahitajika kuwa na vitu vya muhimu kama vile, kitambulisho chenye kuonyesha utaifa, kuwa na sanduku la posta (nitakwambia kwa nini), kuwa na kadi ya benki au akaunti ya benki inayofanya kazi (mwanzoni) pia unahitajika kujua vitu vingine vya msingi kama tarehe yako ya kuzaliwa na vitu vingine kuhusu benki yako kama namba ya utambulisho ya benki yako inayo julikana kama (Swift Code).

Mambo haya ya benki yana hitajika kwa awali unapojiunga na huduma hiyo, ila baada ya kupokea pesa kwa mara kadhaa basi utaweza kupewa kadi maalum kutoka Payoneer ambayo utaweza kutumia kutoa pesa kutoka kwenye ATM zenye MasterCard hapa nchini Tanzania. Kwa hiyo basi, wakati unataka kujiunga na huduma hii unatakiwa kuhakikisha unavyo vitu hivyo hapo juu ili kuweza kupokea muamala wako wa kwanza na baada ya hapo utaweza kutoa pesa zako ukiwa hapa Tanzania. Pia sanduku la posta ni muhimu kwaajili ya kupokea kadi ya ATM ambayo utapokea kutoa nje ya nchi. Kama unataka kujiunga na huduma hii ya Payoneer unaweza kujiunga kwa kubofya hapa.

Kama nilivyo kwambia awali njia hii inatumiwa sana na watu wengi kuweza kupokea malipo mtandaoni kutoka nje ya Tanzania, kama unataka kujua njia za kupokea pesa mtandaoni kutoka nje ya nchi na kuzipata kupitia Mtandao wa simu (M-pesa na Tigo Pesa) unaweza kusoma njia inayofuata hapo chini.

  • Worldremit

Worldremit ni huduma nyingine inayoweza kusaidia kupokea pesa kutoka nje ya nchi, huduma hii inatumiwa sana na watu wengi ambao wako nje ya Tanzania na wanataka kutuma pesa kwa ndugu, jamaa au hata marafiki, huduma hii pia inakupa uwezo wa kutuma pesa ukiwa nje ya nchi na pesa zitamfikia mtu kwa haraka kupitia huduma za kipesa kupitia mtandao wa simu kama vile, Tigo pesa, Mpesa, Airtel Money na nyingine.

Kama nilivyo sema huduma hii hutumiwa na watu wanaotaka kutuma pesa kutoka nje ya nchi kuja Tanzania. Kama wewe una ndugu au jamaa anaye ishi nje ya nchi na unata akutumie pesa na uzipate kwa haraka kupitia simu yako basi huduma hii inafaa sana.

Vilevile Worldremit inawezesha kupokea pesa kupitia mabenki mbalimbali ya hapa Tanzania kama vile matawi ya benki ya The People’s Bank of Zanzibar pamoja na matawi ya benki ya Diamond Trust Bank. Worldremit ni huduma mpya hapa nchini Tanzania, lakini ni huduma ambayo imekuwa ikitumiwa na watu kutoka nchi mbalimbali kwa muda mrefu sana toka mwaka 2010 ilipoa anzishwa rasmi.

Kama unataka kujiunga na huduma hii pia unahitajika kuwa na kitambulisho cha utaifa au kitambulisho chochote kinachotolewa na serikali, pia unahitajika kuwa na namba ya simu iliyo unganishwa na huduma za kutuma na kupokea pesa kwa kutumia simu mfano M-pesa, Tigo Pesa na nyingine, pia unatakiwa kujua vitu vya muhimu vya binafsi kama tarehe ya kuzaliwa, jina la mahali na mtaa unaoishi pamoja na sanduku la posta (Japo sio muhimu sana).

Kama tayari unavyo vitu vyote hivi na ungependa kujiunga na huduma hiyo unaweza kufanya hivyo kwa kubofya hapa. Pia unaweza kupakua app za Worldremit kupitia App Store na Play Store.

Kwa sasa hizo ndio njia mbili ambazo zinaweza kukusaidia kupokea pesa mtandaoni kutoka nje ya nchi kuja Tanzania, kama kuna njia nyingine ambayo unazifahamu unaweza kutufahamisha kupitia sehemu ya maoni hapo chini, tuna ahidi kuongeza njia hizo kwenye list hii. Kumbuka njia hizi zote zinatoza gharama kuwezesha kupata huduma hizo, hivyo ni vyema kusoma vigezo na mashari vya kampuni husika ikiwa pamoja na kujua gharama zinazo tozwa kwa kupokea au kutuma pesa.

11 comments
  1. je Kama kwa Mano umetumiwa pasa kutoka Qatar through tigopesa Lindi muamala unaposoma kwenye account yako wapi pakwenda kuzitoa ni benki au hata kwa mawakala wetu Hawa wa mitaaani?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use