Ulinzi wa iPhone X wa “Face ID” Sio Salama Kama Unavyodhani

Wataalamu wameweza kufungua simu hiyo kwa kutumia picha ya 3D
iPhone-X-Face-ID iPhone-X-Face-ID

Miezi michache iliyopita kampuni ya Apple iltangaza kwenye uzinduzi wa iPhone X kuwa aina mpya ya ulinzi unaotumika kulinda simu hiyo “Face ID” ni salama na imara sababu ulinzi huo hutumia teknolojia ya kisasa kuweza kutambua sura yako ili kufungua simu yako.

Aidha Apple iliongeza kuwa ulinzi huo hauwezi kudanywa kwa kutumia picha ya sura ya mwenye simu…well. Kampuni moja ya ulinzi ya nchini Vietnam imepingana na hayo baada ya kufanikiwa kufungua simu ya iPhone X kwa kutumia mchoro wa pembe tatu (3D) wa sura ya mwenye simu hiyo.

Advertisement

Kampuni hiyo imedai kuwa imefanikisha hilo kwa kutumia picha ya pembe tatu (3D) iliyotengenezwa kwa kutumia material ya silicone pamoja na picha za 2D za macho na mdomo ili kupata mfanano wa sura ya mwenye simu hiyo.

Japokua hatua hii sio rahisi kufanya kutokana na kuitaji mkubwa wa maandalizi pamoja na utaalam wa hali ya juu lakini bado Apple inatakiwa kuboresha ulinzi huo kwani sasa hatua hii inawezekana kwa wale wenye nia za dhati kabisa za kufungua simu hiyo ya iPhone X.

Kwa sasa hatua hii ya kuweza kufunja ulinzi wa Face ID kwa picha ya pembe tatu 3D hauna madhara kwa watumiaji wa kawaida kutokana na ugumu wa upatikanaji wa material ya kuweza kutengeneza picha hiyo, lakini huenda siku za mbeleni ulinzi huu ukawa sio wa kutegemewa sana..

Je wewe unaonaje kuhusu hili unahisi ni ulinzi gani ambao ni bora wa kutumia kwenye simu yako, ambao unadhani unaweza kulinda simu yako vizuri angalau kwa asilimia 90..? tumbie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use