Zifahamu Hizi Hapa Ndio Simu Kumi Bora kwa Mwaka (2018)

Hizi hapa ndio Smartphone bora kwa mwaka huu mzima wa 2018
Zifahamu Hizi Hapa Ndio Simu Kumi Bora kwa Mwaka (2018) Zifahamu Hizi Hapa Ndio Simu Kumi Bora kwa Mwaka (2018)

Mwaka 2017 ndio huo unakaribia kuisha, ingawa bado makampuni mengine ya simu yanaendelea kutoa simu mbalimbali lakini mpaka sasa hizi hapa ndio simu kumi bora kwa mwaka 2017 hadi mwaka 2018.

Kumbuka list hii imepangwa kwa kuzingatia maoni mbalimbali ya watu kupitia tovuti mbalimbali, bila kusahau data za idadi ya mauzo ya simu husika. Basi baada ya kusema hayo basi moja kwa moja twende tukanze list hii.

10. Motorola Moto E4

Advertisement

Motorola Moto E4 ni simu ambayo pengine kwa mwaka huu hatukufanikiwa kuizungumzia, lakini kama wengi wetu tunavyojua kampuni ya motorola imerudi na imekuja na simu bora mbalimbali ikiwemo Motorola Moto E4. Kwa kifupi simu hii ina sifa za kioo cha inch 5.0, RAM GB 2, Ukubwa wa ndani GB 16, Kamera ya Mbele Megapixel 5 na nyuma Megapixel 8 na Mfumo wa Android Nougat 7.1. Simu hii ni moja kati ya simu za bei rahisi sana inanzia dollar $129 sawa na Tsh 300,000.

9. Motorola Moto G5 Plus

Motorola Moto G5 Plus ni simu pia kutoka motorola, simu hii imeshika nafasi ya 9 kwa simu bora zaidi kwa mwaka 2017 ikiwa na sifa za kioo cha inch 5.2, RAM kati ya GB 2 au GB 4 Ukubwa wa ndani kati ya GB 32 na GB 64, Kamera ya Mbele Megapixel 5 na nyuma Megapixel 12 pamoja na Mfumo wa Android 7.0 ambao unaweza ku-update kwenda mfumo wa Android Oreo 8.

8. Motorola Moto Z2 Play

Bado tunaendelea na simu za motorola, kwenye list namba 8 ni simu hii ya Motorola Moto Z2 Play, simu hii imekua bora mwaka huu na sifa zake za kioo cha inch 5.5, RAM kati ya GB 3 na GB 4 pamoja na Ukubwa wa ndani wa GB 64 na GB 32, Kamera ya Mbele Megapixel 5 na nyuma Megapixel 12 ikiwa inakuja na Mfumo wa Android 7.1.1.

7. OnePlus 5

OnePlus 5 ni simu ambazo pengine unaweza usizione sana kwa hapa Tanzania lakini ni kweli kwamba hizi ni moja kati ya simu bora sana. Kwa mwaka huu OnePlus 5 imeshika namba 7 kwa simu bora kwa mwaka 2017 ikiwa na sifa za kioo cha inch 5.5, RAM kati ya GB 8 na GB 6 Ukubwa wa ndani kati ya GB 128 na GB 64, Kamera ya Mbele ya Megapixel 16 na nyuma ziko mbili moja yenye Megapixel 16 na nyingine inayo Megapixel 20. OnePlus 5 inakuja na mfumo wa Android Nougat 7.1.1.

6. Apple iPhone 8

iPhone 8 ni simu mpya kutoka Apple iliyotoka mwaka huu 2017, mbali na watu wengi walivyodhania simu hii imekuja na maboresho machache ambayo ambayo yamefanya simu hii kufikia namba 6 kwenye list hii. Kama unataka kujua sifa za simu hii unaweza kupitia ukurasa Huu.

5. Google Pixel 2

Google Pixel 2 ni simu kutoka kampuni ya Google, kwa mwaka huu kampuni hiyo ilitoa simu hii kwama mfulizo wa matoleo ya simu za Google Pixel yalio anza rasmi hapo mwaka jana. Simu hii iko namba tano kwenye list hii ikiwa na sifa na kioo cha inch 5.0, RAM ya GB 4 ukubwa wa ndani wa GB 64 na GB 128, Kamera ya Mbele ya Megapixel 8 na Kamera ya nyuma ya Megapixel 12.2. Simu hii inakuja na Mfumo wa Android Oreo 8.0.

4. Samsung Galaxy S8 

Galaxy S8 ni simu ambayo ilitoka mwanzoni kabisa wa mwaka 2017 lakini bado simu hii iko kwenye chat na leo kwenye list hii simu hii imeshika namba 4 kwa simu bora za mwaka 2017. Simu hii inakuja na sifa za Kioo cha inch 5.8, RAM ya GB 4 na Ukubwa wa ndani wa GB 64, Kamera ya mbele inakuja na uwezo wa Megapixel 8 na Kamera ya nyuma  ni Megapixel 12. Simu hii inakuja na Mfumo wa Android 7.0.

3. LG V30

LG V30 ni moja kati ya simu zilizo fanikiwa sana kwa mwaka 2017, ijapokuwa inawezekana simu hii haijafika kwa hapa Tanzania lakini ni moja kati ya simu ambazo binafsi yangu ningependa kujaribu kuitumia. Simu hii inakuja na sifa za Kioo kikubwa cha inch 6.0, RAM ya GB 4 na Ukubwa wa ndani wa GB 64 na GB 128, Simu hii pia inakuja na Kamera ya mbele ya Megapixel 5 na Kamera ya nyuma ziko mbili moja inayo Megapixel 16 na nyingine inayo Megapixel 13. Simu hii inakuja na Mfumo wa Android Nougat 7.1.2.

2. Apple iPhone X

iPhone X ni moja kati ya simu iliyofanikiwa sana kwa mwaka huu, Apple imeuza mamilioni ya simu hii ijapokua simu hii imeanza kuuzwa kwa gharama kubwa za kuanzia dollar za marekani $1000 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 2,300,000. Simu hii ina sifa za Kioo cha inch 5.8, RAM ya GB 3 na Ukubwa wa Ndani wa GB 64 na GB 256, Simu hii inakuja na Kamera ya mbele ya Megapixel 7 na Kamera za nyuma ziko mbili zote zinayo Megapixel 12. iPhone X inakuja na mfumo wa iOS 11.1.1.

1. Samsung Galaxy Note 8

Note 8 ndio simu inayo onekana kuwa ni simu bora sana kwa mwaka 2017, simu hii imeonekana kutumiwa na watu wengi wanaopenda simu za Android na imeonekana kusifiwa sana kutokana na sifa zake za Kioo cha kikubwa cha Inch 6.3, RAM ya GB 6 na Ukubwa wa ndani wa GB 64 GB 128 pamoja na GB 256, Note 8 inakuja na Kamera ya mbele yenye Megapixel 8 na kwa nyuma inakuja na Kamera mbili zote zikiwa zina Megapixel 12. Simu hii inakuja na Mfumo wa Android Nougat 7.1.1 ambao unaweza kufikia mpaka mfumo wa Android Oreo 8.0.

Na hizo ndio simu bora kwa mwaka huu 2017, kumbuka list hii inatokana na maoni ya watu mbalimbali kupitia mitandao mbalimbali mikubwa ya habari na makala za teknolojia. Kwa kuzingatia hayo je wewe unaonaje..zipi ni simu bora kwako kwa mwaka 2017..? tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

11 comments
  1. Kuna Simu Nyie balaaa Kama Gooe NEXUS 6 Mbna.hamjaziandika.mnatuwekea motolora 8MP camera c bora ungeweka hata phantom 8 tjkajua 1

  2. m naona hyo list iko mkide sana ila naomba na bei yake mweke kwa kila simu mtu ajue anaanzia wap

  3. Toa listi ya cm za sasa sio mwaka Jana kila mda cm znatoka mpya unaleta ya mwaka Jana au mnakula mb bure

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use