Huawei Yazindua Huawei Nova 2S Simu Mpya Yenye Kamera Nne

Simu hiyo mpya imezinduliwa rasmi huko nchini China
Huawei Yazindua Huawei Nova 2S Simu Mpya Yenye Kamera Nne Huawei Yazindua Huawei Nova 2S Simu Mpya Yenye Kamera Nne

Kwa muda wa miezi michache iliyopita huawei imezundua simu za Mate 10/Mate 10 Pro, Honor View 10, pamoja na Honor x7. Lakini kama haitoshi Huawei wamerudi na simu nyingine ya Huawei Nova 2s simu ambayo imezinduliwa muda si mrefu huko nchini china.

Huawei Nova 2S ni muendelezo wa matoleo ya simu za Huawei Nova na Nova Plus ambayo yalianza kutoka rasmi hapo mwaka jana. Simu hii ya sasa ya Huawei Nova 2S inakuja na maboresho mapya pamoja na kioo kikubwa kisicho na mipaka.

Kwa mbele simu hii ina kioo cha inch 6 chenye ukubwa wa 2160 x 1080, simu hii ina aspect ratio inayotumiwa na simu nyingi kwa sasa ya 18:9, lakini pamoja na wembamba wake kutoka ukingo wa juu mpaka kwenye kioo bado Huawei wameweza kuweka kitufe cha Home ambacho kinatumika pia kama sehemu ya ulinzi ya fingerprint.

Advertisement

Simu hii Mpya ya Huawei Nova 2S inakuja na Mfumo tofauti kidogo wa kamera, Simu hii ina kamera mbili za nyuma moja yenye uwezo wa Megapixel 16 ikiwa na uwezo wa color sensor na nyingine inayo megapixel 20 yenye uwezo wa monochrome one na f/1.8 aperture.

Haija ishia hapo simu hii inakuja na Kamera za mbele mbili moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 20 yenye f/2.0 aperture, na nyingine ikiwa na uwezo wa megapixel 2 huku zote zikisaidia na Flash iliyoko mbele ya LED flash.

Kwa upande wa processor simu hii inakuja na processor yenye nguvu ya Kirin 960 processor, RAM ya 4 GB pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 na GB 128, Kwa mfumo simu hii inakuja na mfumo mpya wa Android 8.0 Oreo vyote hivyo vikiwa vinaendeshwa na Battery yenye uwezo wa 3,340 mAh ambayo inaweza kudumu na chaji kwa siku nzima bila wasiwasi.

Unaweza kupata simu hii kwa bei ya dollar za marekani $400 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 900,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya leo (kumbuka bei inaweza kubadili kwa Tanzania). Vilevile simu hii inakuja kwa rangi tano za Black, Gray, Red, Blue, pamoja na Rose Gold.

Simu hii inategemewa kuanza kupatikana rasmi kuanzia mwakani na kwa hapa Tanzania, Tunaweza kuanza kuipata kuanzia mwezi wa pili au wa tatu hapo mwaka 2018.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use