Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Twitter Yawataka Watumaji Wake Kubadili Password (Nywila)

Ni muhimu kuhakikisha akaunti yako inakuwa salama kwa kufanya hivyo
Twitter Yawataka Watumaji Wake Kubadili Password (Nywila) Twitter Yawataka Watumaji Wake Kubadili Password (Nywila)

Mapema siku ya jana mtandao wa Twitter kupitia ukurasa wake wa Twitter Support uliandika kuwa, kwa sababu za usalama inashauri watumiaji wa mtandao huo kuchukua hatua za mapema na kubadilisha Password au nywila za akaunti zao ili kulinda akaunti zao kuweza kudukuliwa.

Habari kupitia blog ya Twitter zinasema kuwa, wabunifu programu wamegundua tatizo kwenye mfumo wa password wa Twitter ambapo password zinaweza kuhifadhiwa bila kufichwa na hivyo kuezesha wabunifu hao kuweza kuona password za akaunti yako pale unapotumia mtandao wa Twitter au unapoingia kwenye tovuti au programu mbalimbali kwa kutumia Twitter.

Advertisement

Kupitia post hiyo Twitter imeeleza kuwa, inatumia mfumo wa kuficha password unaoitwa bcrypt, ambao unahifadhi password kwa kubadilisha namba na herufi unazotumia kwenye password yako na kuwa maaandishi ambayo hayasomeki na hivyo kuwezesha kuficha password yako kuonekana na wabunifu mbalimbali wa tovuti au programu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Twitter mfumo huo umegundulika kuwa na tatizo kwani, kabla ya mfumo wa bcrypt kufanya kazi yake ya kuficha password yako, password hizo huifadhiwa pembeni kwenye file maalum kitendo ambacho akikutakiwa kufanyika hivyo kuleta hatari ya kusababisha wabunifu wa tovuti na programu mbalimbali (ikiwa pamoja na Twitter wenyewe), kuweza kupata au kuona password ya akaunti yako hasa pale unapo ingia kwenye mtandao wa Twitter, au hata kwenye programu mbalimbali zinazo ruhusu kuingia (login) kwa kutumia mtandao huo.

Kwa sasa Twitter imeripoti kuwa, tayari imeshafanya marekebisho ya mfumo huo na bado hakuna ripoti zozote zinazo onyesha kama kuna akaunti yoyote iliyo dukuliwa au kuadhiriwa kwa sababu ya matatizo ya mfumo huo. Mbali na hayo Twitter imewataka watumiaji wote kuweza kubadilisha Password za akaunti zao ili kuweza kulinda akaunti zao zaidi.

Hivyo basi kama unahisi akaunti yako imekua na tabia usiyo elewa basi ni wakati wa kubadilisha password yako na pia unaweza kuongeza ulinzi zaidi kwenye akaunti yako kwa kufuata njia za Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuhack akaunti zako za mitandao ya Twitter, Facebook pamoja na Instagram.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use