Sasa Utaweza Kuangalia Fainali za UEFA Kupitia YouTube

Sasa fainali za kombe la UEFA Champions League ni kupitia YouTube
UEFA UEFA

Mpira wa miguu ni moja kati ya mchezo unaopendwa zaidi duniani na imekuwa ni kawaida kuangalia mchezo huu kupitia vingamuzi au channel mbalimbali za kulipia, lakini mwaka huu hali itakuwa tofauti kidogo. Fainali za UEFA Champions League zimekuwa zikirindima kila mwaka mwezi May na mwaka huu utaweza kuangalia mchezo huo unaotegemewa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mubashara kabisa kupitia mtandao wa YouTube.

Fainali hiyo kati ya timu za Liverpool na Real Madrid zitakuwa mubashara siku hiyo kupitia channel ya BT Sport’s YouTube channel. Zaidi ni kuwa fainali hizo zitaonyeshwa kwenye mfumo wa 4K, yaani maana yake ni kuwa kama una kifaa chenye uwezo wa 4K basi utaweza ku-enjoy mchezo huo utakao fanyika jumamosi ya wiki ijayo.

“Tumekuwa tunasema kuwa tunataka kufanya michezo ya hali ya juu kupatikana kwa watu wengi na kwa mara nyingine tena tutafanya fainali za UEFA Champions League na Fainali za Europa League kupatikana kuangalia mtandaoni bure,” Msemaji wa BT Sport alinukuliwa akisema.

Advertisement

Hata hivyo siku ya jana Channel hiyo ya Youtube ya BT Sports, ilionyesha mchezo wa fainali za Europa League mubashara kupitia channel yao hiyo. Kwa bahati mbaya video hiyo kwa sasa huwezi kuiangalia kama uko nchini Tanzania, lakini unaweza kutumia programu za VPN kuweza kuangalia video hiyo kwa nchi zilizo ruhusiwa. Baada ya kuinstall VPN kwenye Simu au Kompyuta yako unaweza kuangalia video kwa kubofya hiyo hapa.

Kama wewe ni mpenzi wa mpira wa miguu basi, endelea kutembelea Tanzania Tech, tutangalia uwezekano wa kuweka video hiyo hapa ili wote tuweze kufurahia mchezo huo wa fainali siku ya Tarehe 26 ya mwezi huu wa tano.

6 comments
  1. shukran kwa kazi nzuri unayoifanya ila hiyo vpn tutaipataje kwa kweli manake hatujaijuwa na inapatikana play stor ndugu yetu?hem tusaidie kwa hili

    1. Ndio kama unatumia Simu ingia Play Store kisha tafuta VPN pakua app yoyote yenye nyota nyingi kisha install kwenye simu yako. Baada ya hapo njoo kwenye makala hii kisha bofya link hapo juu kuangalia video hiyo.

      1. nimedanlod vpn na nikaja kwenye hiyo link hapo kwako lakini nayo haijafunguka unahisi nn tatizo

        1. then nimeangalia vpn zote unachaguwa nchi lakini ukichaguwa Tanzania au Africa hamna hata nchimoja sasa inakuwaje kiongozi au naomba kama itawezekana unitumie angalau picha tu ya vpn ambayo ww unatumia kuona ili nidanlod kama yako unayotumia

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use