Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kama Wewe ni Mtumiaji wa Mtandao Simu wa Halotel Soma Hii

Sasa unaweza kuwasiliana bila kikomo
Halotel Halotel

Hivi karibuni Kampuni ya Halotel imezindua kifurushi kisichoisha kitakacho wawezesha wateja kufanya mawasiliano bila kikomo. Wateja wa Halotel watakao jiunga na kifurushi hicho kipya kiitwacho Super Halo, watapiga simu au kutumia intaneti hadi kitakapokwisha bila kujali muda wa kujiunga.

Mkuu wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Mhina Semwenda amesema kifurushi hicho kinaondoa ukomo wa muda wa vifurushi vya maongezi na intaneti. “Huu ni ubunifu katika huduma zetu ili kuwawezesha wateja kunufaika na mawasiliano bila wasiwasi wa kuisha muda wa matumizi walionao kwenye simu, hivyo kukidhi mahitaji yao kijamii na kiuchumi,” amesema Semwenda.

Advertisement

Amesema mteja anaweza kujiunga kuanzia Sh500 na kuendelea. Kwa sasa kampuni nyingi za simu huwa na vifurushi vyenye ukomo kwa mfano saa 24, wiki au mwezi ambavyo hata kama mteja hakutumia simu muda huo ukishapita salio husika haliwezi kutumika tena.

Mbali na kifurushi hicho, Halotel imezindua Facebook ya bure ambayo kuanzia sasa wateja wa mtandao huo wataweza kuperuzi bila kulipia gharama zozote. Kwa sasa bado hatujapata taarifa zaidi juu ya jinsi ya kujiunga hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech, tutakujulisha pindi tutakapo pata taarifa jinsi ya kujiunga na kifurushi hicho cha Super Halo.

Makala Imeongezwa Tarehe 15-05-2018 Saa 4:49

Tumefanikiwa kupata Aina ya Vifurushu utakavyoweza kujiunga, ikiwa pamoja na Bei halisi za vifurushi hivyo. Pia ili kujiunga na SupaHalo bofya *148*66#.

5 comments
  1. Mimi nimeshaanza kunufaika na huduma hiyo tangu wiki iliyopita, ni huduma nzuri sana na inaondoa kero ya vufurushi kuwa na ukomo, natamani ma makampuni mengina ya simu kuwa kama wao halotel.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use