Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tukumbushane : Sheria za Makosa ya Mitandaoni na Adhabu Zake

Kama umeshau kidogo sheria za makosa ya mitandaoni basi soma hii
Makosa ya Mtandaon Makosa ya Mtandaon

Hivi karibuni kumekua na mijadala mbalimbali kuhusu sheria za makosa ya mtandaoni, sheria ambazo zilitungwa na kupitishwa na bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania hapo mwaka 2015, lakini sheria hizi ni watu wachache sana wanazijua au wanajua mahali pakuzi pata ili kuweza kuzisoma basi leo Tanzania Tech tunakuletea makala hii ya sheria hizo na adhabu zake.

Kwa mujibu wa blog ya michuzi blog mambo yafuatayo ndio baadhi ya mambo muhimu ambayo ni muhimu kuyajua kama unataka kuwa salama na kujiweka mbali na adhabu inayotokana na makosa ya mtandaoni.

Advertisement

  • Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao.
  • Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza
    kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao.
  • Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k ).
  • Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii.
  • Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea) itakugharimu.
  • Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu.
  • Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu.
  • Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu.
  • Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini.
  • Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia ‘brand’ ama jina la mtu itakugharimu.

Hayo ni baadhi ya mambo tu ambayo ni muhimu sana kuzingatia sana kwenye sheria za makosa ya mitandao, kusoma sheria zote kamili na adhabu zake unaweza kudownload sheria hizo zilizoko kwenye mfumo wa pdf hapo chini, sheria hizo zipo kwa kiswahili na kingereza kiswahili kipo mwisho kabisa wa document au hati hiyo.

SHERIA ZA MAKOSA YA MTANDAONI

Bila shaka utakuwa upata kujua au kujikumbusha baadhi ya sheria ambazo kwa namna moja ama nyingine ulkua umesahau, kama una swali au maoni unaweza kutuandikia hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Mst.go.tz, Michuzi Blog

15 comments
  1. Mmesema kiswahili napata wapi mbona sioni sehemu ya kiswahili? Nataka sheria ya makosa ya kimtandao

    1. Ndio, sithani kama sheria inaruhu swala hilo, pia ni vyema kusoma sheria hizo ili kujua zaidi.

  2. Hapo sawa sheria itasimamia haki yake pamoja Na kushugulukia wanaokiuka sheria ususani kwenye mitandao Na kuzuia wizi Mara kwa Mara

  3. Vitu gani vinaitajika ikiwa umepotea simu yako au kopyuta unapolipoti kwa mamlaka husika uweze kupata Mali zako kiurahisi??

    1. Nadhani hatua ya muhimu ni kutoa ripoti kupitia kituo cha polisi hapo utaweza kupewa utaratibu mwingine.

  4. Naomba kujua athabu ya mtu kuchukia picha za mtu bila rizaa yake nakuzipost kwenye mitandao yakijamii kwa kumchafua kuwa ni tapeli nk bila…athabu yake huwa Ni Nini.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use