Jinsi ya Kufanya Simu za Tecno Kudumu na Chaji Zaidi (2019)

Chaji simu ya tecno kwa kufuata njia hizi utaona mabadiliko makubwa
Simu za Tecno kudumu na Chaji Simu za Tecno kudumu na Chaji

Wote tunajua kwa hapa Afrika na Tanzania kwa ujumla simu za tecno ni moja ya simu zinazotumiwa sana, lakini simu hizi huwa na matatizo mbalimbali na moja kati ya tatizo hilo tutaenda kuliongelea leo ambalo ni kuisha kwa chaji haraka.

Mara nyingi hatua za kudhibiti chaji kupungua kwenye simu za tecno ni sawa na zile za kudhibiti kupungua kwa chaji haraka kwenye simu nyingine, lakini njia tutakazo ongelea hapa nyingi zitakuwa zikihusisha simu za tecno. Unaweza pia kujaribu njia hizi kwenye simu yako ya kawaida ya Android.

  • Punguza Sauti ya Muito

Simu nyingi za tecno zimetengenezwa kwa kutumia spika spesheli, ambazo mara nyingi spika hizi huwa kubwa tofauti na simu nyingine, mara nyingi kutokana na ukubwa wake, spika hizi pia hutumia kiasi kikubwa cha chaji ya ziada pale zinapo toa mlio hivyo kufanya chaji ya simu yako kuisha kwa haraka. Ni vyema kuakikisha sauti ya muito wa simu yako iko kwa kiasi cha kawaida kupunguza matumizi ya ziada ya chaji.

Advertisement

  • Safisha Battery ya Simu yako au Chaji ya Simu Yako

Hapa kuna njia mbili tofauti kwa simu mbili tofauti, Kama simu yako inatoka battery au kama simu yako inafunguka kwa nyuma sehemu ya Battery ni vyema ukachukua muda wako kutoa battery ya simu yako na kusafisha kwenye vikoili vya mbele vya battery yako vinavyo gusana na sakiti ya simu yako. Hii itasaidia kuondoa uchafu unaoweza kuzuia chaji kwenye simu ya tecno kuingia vizuri ndani ya battery ya simu yako.

Vilevile kama huenda simu yako haifunguki kwa nyuma sehemu ya kuweka battery, basi unaweza kusafisha kichwa cha waya wa chaja ni hii itasaidia endapo kuna uchafu unaozuia battery yako kuingia chaji vizuri pale unapochaji.

  • Chaji Simu yako huku umewasha (Flight Mode)

Sehemu ya flight mode ipo kwenye kila simu, sehemu hii itakusaidia kuzima network kwenye simu yako ya pale unapokua unataka kutumia simu yako bila kuwa na mawasiliano ya kimtandao. Sasa ukichaji simu yako uku umewasha sehemu hii inaruhusu simu yako kujaa chaji vizuri kwani chaji inayo ingia haitumiki kwa kasi kubwa na hivyo battery kujaa chaji kwa haraka zaidi na kikamilifu.

  • Hakikisha Simu yako Inaisha Chaji Ndipo Uchaji Tena

Hakikisha smu yako inaisha chaji ndipo uchaji tena, njia hii ni muhimu sana kwani inasaidia battery yako kuweza kudumu zaidi kwani kuisha kwa battery yoyote ndipo kunapo tegemeana sana na kudumu kwa chaji ya battery.

Yaani fikiria hivi, “maji yakikaa sana huaribika na ili kupata maji fresh ni vyema umwage kwanza yake yalio kaa kwa muda mrefu na ndipo uweke maji mengine masafi, kwa mtindo huo maji hayo mapya yatadumu zaidi kuliko kuongezea maji masafi juu ya maji ambayo yalikuwa yamesha kaa kwa muda mrefu” hivyo ndivyo battery ya simu inavyo fanya kazi, hakikisha angalau kila baada ya siku mbili una hakikisha battery ya simu yako inaisha kabisa ndipo uchaji upya.

  • Usichaji Simu yako Kwenye Joto Kali

Kwa wale ambao tunaishi Dar es salaam, najua kuwa joto ni kali ndio maana hapa Dar es salaam simu nyingi zinaharibika battery kuliko hata mikoani, japo kuwa hii inategemeana na ubora wa battery lakini ni kweli kuwa kuchaji battery mahali kwenye joto kali sana husababisha battery ya simu yako kuharibika haraka. Sasa basi ili kudhibiti simu yako ya Tecno kuisha chaji hara na battery yako kuharibika, hakikisha unachaji simu yako ikiwa haijavikwa kava na ni vizuri kuchaji kwenye soketi ya umeme isiyo na msongamano wa vitu vingi.

  • Punguza Matumizi ya Programu Zisizokuwa na Ulazima

Kama kwenye simu yako ya tecno kuna programu nyingi basi ni lazima simu yako itakuwa inaisha chaji mara kwa mara. Ili kuhakikisha kuwa battery ya simu yako ya tecno inadumu zaidi hakikisha unaondoa programu zisizo na ulazima na acha zile ambazo una matumizi nazo ya kila siku. Unaweza kuondoa programu ambazo huzitumii kila siku na pale unapo ziitaji unaweza kuzipakua tena kuliko kubaki nazo kwenye simu bila matumizi ya muhimu ya kila siku.

  • Hakikisha Bluetooth, GPS (Location) na Wi-Fi Zimezimwa

Programu nyingi mbalimbali huwa na uwezo wa kuwasha GPS au Location bila hata wewe kujua, sasa mara nyingi unapo maliza kutumia programu hizi GPS huendelea kuwaka hivyo kutumia kiasi kikubwa sana cha data, pamoja na chaji bila hata wewe kujua. Hii ni moja kati ya zile sababu kwanini unakuta kifurushi chako cha data au (Bando) kimeisha bila hata wewe kutumia.

Na hayo ndio mambo ambayo ni ya msingi sana kuyafanya kama unataka simu yako ya tecno iweze kudumu na chaji, baadhi ya mambo unaweza kuyafanya kwenye simu yoyote ya Android ili kuweza kuongeza ufanisi wa battery yako pamoja na kudumu kwa chaji kwa simu yako.

2 comments
  1. Elimu nimeipenda mkuu ndio maana mdau wa mdamrefu ila nakupongeza kati ya juhudi ambazo umetupatia nasi tunazifatilia na kuwapa na wengine wasiofahamu

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use