Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com

Sasa tumia facebook kwenye kompyuta ikiwa na muonekano mpya kabisa
Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com

Mwaka jana 2019 kupitia mkutano wa F8, Kampuni ya Facebook ilitangaza kuja na mabadiliko mengi sana ikiwa pamoja na mabadiliko makubwa ya muonekano wa website yake ya facebook.

Hivi karibuni kampuni ya facebook imetangaza kuwa sasa watumiaji wake wanaweza kujaribu muonekano mpya wa tovuti ya facebook ambao unapatikana kwa watumiaji wote. Muonekano huo umeboreshwa zaidi na unakuja na sehemu mpya mbalimbali ikiwa pamoja na sehemu ya Dark Mode ambayo sasa inapatikana kwenye programu mbalimbali ikiwa pamoja na WhatsApp.

Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com

Advertisement

Kwa sasa muonekano huo unapatikana kupitia tovuti ya facebook.com hivyo unaweza kujaribu muonekano huo kama unatumia kompyuta. Muonekano huo umerahisishwa zaidi na unakupa nafasi ya kutosha kuweza kufanya mambo mbalimbali kwa urahisi.

Ili kuwasha muonekano huo ingia kwenye tovuti ya facebook.com na moja kwa moja nenda kwenye sehemu ya profile yako karibu na settings bofya hapo na angalia mwisho wa menu hiyo na moja kwa moja unaweza kuona sehemu mpya imeandikwa “Switch to New Facebook“.

Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com

Baada ya kubofya hapo moja kwa moja utapelejwa kwenye ukurasa mpya wenye muonekano mpya wa Facebook wenye mambo mengi mapya. Kizuri ni kuwa, kama unaona muonekano huo sio mzuri kwako unaweza kurudisha muonekano wa zamani kwa urahisi.

Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com

Kama unavyoweza kuona, sasa muonekano wa facebook.com umebadilika kabisa na sasa utaweza kupata nafasi ya kufanya mambo mengi zaidi kuliko hapo awali. Muonekano huo pia unakuja na sehemu mpya nyingi, lakini sehemu ambayo nadhani inaweza kumvutia karibia kila mtu ni sehemu mpya ya Dark Mode.

Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com

Sehemu hii inawezeshwa kwa urahisi kupitia sehemu ya menu iliyojificha juu mwisho upande wa kulia kwenye mshale ulio angalia chini, kwa kubofya hapo na kuangalia mwisho wa menu hiyo utaweza kuona sehemu iliyo andika “Dark Mode“. Bofya kwenye switch hiyo na moja kwa moja utaweza kuwasha muonekano wa giza kwenye tovuti mpya ya facebook.com.

Sasa Jaribu Muonekano Mpya wa Tovuti ya Facebook.com

Pia chini ya sehemu hiyo ya kuwasha Dark Mode, utaweza kuona sehemu ya kurudisha muonekano wa zamani wa facebook kama utakuwa unaona huwezi kutumia muonekano huo mpya. Sehemu hiyo imeandikwa “Switch to Classic Facebook”. Kwa kubofya hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye muonekano wa zamani wa facebook.com.

Kwa sasa watumiaji wote wa mtandao wa facebook kwa njia ya kompyuta wanaweza kujaribu muonekano huo moja kwa moja. Kama wewe ni mmoja wapo basi jaribu muonekano huo kisha tuambie umeonaje muonekano huo mpya wa tovuti ya Facebook.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use