Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuona Idadi ya Maambukizi ya Corona (COVID-19)

Sasa utaweza kujua idadi ya maambukiz ya COVID-19 kwa urahisi
Jinsi ya Kuona Idadi ya Maambukizi ya Corona (COVID-19) Jinsi ya Kuona Idadi ya Maambukizi ya Corona (COVID-19)

Kivinjari cha Opera mini ni moja kati ya (Browser) kivinjari kinacho tumiwa na watu wengi zaidi hasa hapa Tanzania. Kivinjari hicho kinakuja na sehemu ambazo zinamsaidia mtumiaji kufanya mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kupata habari kupitia sehemu mpya ya Opera News.

Hivi karibuni watumiaji wa App ya Opera News na watumiaji wengine duniani wataweza kuona sehemu mpya ya kuweza kutambua Idadi ya Maambukizi ya Corona Live. Sehemu hii mpya itaweza kuonyesha idadi ya maambukizi hayo ya Corona au COVID-19 mubashara kabisa, sehemu hii inasemekana kuwa inabadilika pale idadi hiyo ya maambukizi itakapo thibitishwa na WHO pamoja na wizara za afya za nchi husika ikiwa pamoja na vyanzo vingine mbalimbali.

Advertisement

Jinsi ya Kuona Idadi ya Maambukizi ya Corona (COVID-19)

Mbali na kupata sehemu hiyo kupitia app ya Opera News na Kivinjari chake, pia watumiaji wengine kote duniani wanaweza kuona sehemu hiyo kwa kutembelea link maalum kwenye vifaa vyao. Kwa kutumia link hiyo utaweza kuona Idadi ya Maambukizi ya Corona kwa nchi uliyopo moja kwa moja. Unaweza kutembelea link hapo chini kuangalia sehemu hiyo kwenye kivinjari chochote.

Bofya Hapa Kujua Idadi ya Maambukizi ya Corona

Mbali na njia hiyo, pia Google inakuja na sehemu ya kuonyesha idadi ya maambukizi ya corona kupitia sehemu ya kutafuta (Search Engine). Kwa kuandika neno “virusi vya corona” kwenye sehemu ya kutafuta kwa Google, chini kidogo ya matokeo ya neno hilo utaweza kuona list ya nchi mbalimbali ikiwa pamoja na nchi uliyopo kwa muda huo.

Jinsi ya Kuona Idadi ya Maambukizi ya Corona (COVID-19)

Kama ilivyo app ya Opera News, sehemu hiyo pia inatoa data zake kupitia sehemu ya WHO pamoja na wikipedia. Kwa sasa sehemu zote zinapatikana kwa watumiaji wote dunia nzima na unaweza kujaribu sasa kuona idadi ya maambukizi ya corona kwenye nchi uliyopo sasa.

1 comments
  1. Naomba kujinga na app yenu kwasababu no app inayohabarisha Mambo ya ukweli na yanayoelimisha jamii.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use