Kama wewe ni mmoja wa watu ambao ungependa kutengeneza pesa mtandaoni kuanzia $5 na kuendelea basi pengine njia hii inaweza kufaa sana kwako.
Kupitia njia hii nitaenda kuonyesha tovuti ambayo inaweza kukulipa kutokana na kutoa maoni kwenye programu na biashara mbalimbali mtandaoni. Biashara au programu hizo ni pamoja na programu kama WhatsApp, Telegram, Canva na programu nyingine.
Kitu cha muhimu unatakiwa kuhakikisha unatoa maoni ya kweli, na pia unatakiwa kuwa umeshawahi kutumia programu hiyo au tovuti.
Ni rahisi kufanya review na huitaji vitu vingi zaidi ya kuwa na akaunti yako ya Google au barua pepe yoyote na pia hakikisha pia unayo internet kwenye kifaa chako. Kama tayari unavyo vyote hivyo basi moja kwa moja twende kwenye njia hii.
Kwa kuanza unatakiwa kutembelea tovuti hapo chini, baada ya kutembelea bofya kitufe cha SignUp na kisha tengeneza akaunti kwa kutumia akaunti yako ya Google kwani hii ni rahisi zaidi au unaweza kutumia barua pepe yoyote.
Tembelea Tovuti Hapa (Updated)
Baada ya kuingia kumaliza kujisajili utapelekwa moja kwa moja kwenye Dashboard na hatua inayofuata ni kubofya kitufe cha “Software Used”.
Baada ya kubofya sehemu hiyo utaletewa ukurasa wa kufafuta na hapa unatakiwa kutafuta programu yoyote au website ambayo umewahi kutumia. Unaweza kutafuta programu ya WhatsApp au programu nyingine yoyote.
Kwenye Matokeo chagua programu ya WhatsApp kisha shuka chini kidogo utaona sehemu ya kuandika maoni kuhusu programu ya WhatsApp. Moja kwa moja bofya “Write A Review”.
Baada ya hapo fomu itafunguka na unatakiwa kujaza majina yako kamili, hakikisha majina hayo ni sahihi. Kisha moja kwa moja anza kujibu maswali kuhusu programu ya WhatsApp. Maswali ni marahisi sana na unaweza kujibu kulingana na matumizi yako.
Baada ya kumaliza maswali yote moja kwa moja subiri na baada ya muda mfupi au baada ya siku moja moja kwa moja utaweza kutumiwa barua pepe yenye kukupa zawadi yako kulingana na review yako. Unaweza kupokea malipo kama gift card au kwa njia unayo ipendelea.
Kama unavyoweza kuona hapo juu hii ndio barua pepe ambayo utapokea ikiwa pamoja na link maalum ya kuchukua zawadi yako moja kwa moja. Njia hii ina uhakika wa asilimia 100 na ni salama na uhakika. Kitu cha muhimu hakikisha utengeneza akaunti na barua pepe ya ukweli na unajibu maswali yote kwa usahihi.
Kwa kufanya njia hii natumaini utakuwa umeweza kutengeneza angalau $5 kupitia mtandao. Kama kwa namna yoyote umekwama unaweza kuuliza kupitia maoni hapo chini. Pia kama unataka kujifunza zaidi njia za kutengeneza pesa mtandaoni hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
vp kuhusu fursa za cryptocurrency kama vile metaforce pia naiona ni nzuri sana hivyo ingelikuwa vizur mkatoa mafunzo yake
Link haifunguki shida Nini
Mbona link inafanya kazi..? Unatumia app ya Tanzania Tech app unatumia Browser..?