Namna ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni kwa Mwaka 2020

Jipatie Kipato Mpaka TZS 500,000 kwa Mwezi Kwa Kufanya Biashara Hii
biashara mtandaoni biashara mtandaoni

Watu wengi hudhani ya kwamba kuanzisha bishara ni lazima uwe na mtaji mkubwa au uwe na sehemu ya kufanyia biashara lah! hasha kwa kutumia akili na kwa kufuata ratiba yako kila siku unaweza uanzisha biashara kwa kiasi kidogo sana cha pesa na ukajipatia faida kemkem baada ya mda mfupi.

Leo sitaenda kukudanganya kwamba eti utatengeneza mamilioni kwa muda mfupi kazi hii inaitaji ustarabu na inaitaji uwe mpenda mitandao na bila kusahau uwe na nia, watu wengi hudhani eti kwa sababu ni biashara ya mtandaoni basi unakua unafanya pale tu unapojisikia ningependa kukwambia tu ili kufanikiwa jambo lolote ni vyema kwanza ukawa na nia nalo na ufanye kwa nguvu zote pamoja na akili zako zote.

Advertisement

Moja kwa moja basi twende nikakufundishe kuanza biashara yako ambayo nauhakika ukiifanya kwa umakini na kwania utapata mara kumi ya kiasi ulichotumia kuanza biashara hii. Bila kupoteza wakati twende tukaone ni vitu gani unavyoitaji ili uweze kufanya biashara  yako kwa mtaji wa elfu 19,000 tu. Moja kati ya vitu unavyotakiwa kuwa navyo ni Computer iwe unatumia laptop au desktop unaweza kuanza biashara hii bila wasiwasi wowote lakini jitahidi sana uwe na laptop kwani hii ina amishiaka na nirahisi kwenda nayo mahali popote hata kama ni kazini au safarini.

Pia jitahidi uweze kuwa na modem au kama huna modem basi uwe na smartphone yako ambayo unaweza ukatumia kama modem kwenye computer yako, pia jitahidi uwe unapata internet hata mara tatu kwa wiki kwani itakusaidia kufuatilia biashara yako na pia kutafuta masoko ya biashara yako. Kingine cha muhimu sana jitahidi uwe una akaunti za mitandao ya kijamii kwani hapa ndo penye siri ya biashara yenyewe, ukiwa na vitu hivi utakuwa uko tayari kuanza biashara hii rahisi ambayo haitaji ujuzi wowote ule.

Haya sasa baada ya kuwa na hayo yote moja kwa moja ingia katika tovuti hii Hapa hakikisha unatumia tovuti hiyo na si vinginevyo kwani kwa kutumia tovuti hii ndipo mahali pekee unapoweza kuanza biashara yako hiyo kwa kiasi hicho cha Tsh 19,000 tu. Baada ya hapo utaletwa kwenye tovuti hiyo ikiwa na maelezo ya kukushawishi wewe kuanzisha website au blog ikiwa pamoja na bei za vifurushi mbalimbali, kumbuka usiogope kwani huna haja ya kuwa blog au kumuajiri website designer ili kusudi ufanye biashara hii cha msingi ni kufuata maelezo haya hatua kwa hatua bila kukosea.

Baada ya hapo chagua kwa kubofya neno “select” kwenye kifurushi chakwanza ambacho kinaitwa “Starter” ambacho ni chakwanza kutoka upande wa kushoto kisha baada ya hapo utaletwa mahali ambapo unatakiwa kuchagua jina la domain yako ambapo hili ndilo litakua jina la website yako kama wewe ungepende pia kufanya au kutengeneza blog chagua jina blog yako ambalo litaendana na kitu ambacho unataka kukifanya sasa au hata baadae hakikisha unachagua jina makini.

Baada ya hapo chagua Domain yako kisha nenda kwenye malipo jaza jina lako kamili pamoja na mambo mengine kama inavyotakiwa na kisha lipia kiasi hicho cha Tsh 19,000 alafu sasa hapo utakuwa karibia unaaza biashara yako kwa urahisi kabisa. Hapa nakupa SIRI utakapo tumia kiasi hichi cha Tsh 19,000 kwa kupitia tovuti hiyo hapo juu utaanza moja kwa moja kwa kujipatia kiasi cha Dollar za kimarekani $2  hizi ni kwaajili tu ya asante ya kujiunga na mtandao huo. Namana ya kuangalia kiasi hicho cha hela nenda upande wa kulia juu kabisa kwenye kona utaona neno “Earn Money” hapa ndipo sehemu utakayo weza kuona ni kiasi gani ulilichopata na pia hapa ndipo biashara yetu huanzia.

Chukua Link iliyoandikwa “Your referral link” kisha copy na uituze mahali kwani huu ndio mfreji wetu wa pesa baada ya hapo soma maelekezo yaliyoko kwenye ukurasa huo kwa makini ambayo kwa kifupi yanasema kwamba kwa kila mteja utakaye mleta utaweza kujipatia kirahisi kiasi cha dollar za kimarekani $10, na pindi unapoleta wateja watano ambayo ni sawa na dollar $50 hapo utaweza kutoa pesa zako kwenda kwenye account yoyote duniani pia kwa kila mteja aliye letwa na link yako atajipatia kiasi cha dollar za kimarekani $2 rahisi eh!.

Ile link uliyo copy ndio wateja wako watakayo tumia kuingilia katiaka tovuti ili wajipatie na wao pesa, hapo najua unajiuliza utaipost wapi link hiyo unaweza kuipost link hiyo kwenye group au hata kwenye profile yako ya instagram kisha andika alezea watu naman ya kufanya kisha acha hapo na usubiri hela zimiminike.

UPDATE

Kutokana na watu wengi kuuliza kama hii ni kweli ama si kweli, picha hiyo hapo chini inaonyesha malipo yetu ambayo bado hatuja chukua kuanzia Mwezi march Mpaka sasa.

screenshot

Kama unataka maelezo zaidi unaweza ukapitiaa video hiyo apo juu yenye ushaidi wa akaunti yetu baada ya kupata pesa hapo awali mwaka huu.

Update – 2019 Kutengeneza Pesa mtandaoni kuna hitaji uvumilivu na unatakiwa kuamini hii ni kazi kama kazi nyingine, ukizingatia utafanikiwa. Gharama za kuanza biashara hii zina tegemeana na viwango vya kubadilisha fedha vya siku ambayo unajiunga, hivyo gharama zinaweza kuongezeka zaidi ya Tsh 19,000.

Usisite Ku-comment kama unataka maelezo zaidi na kama unataka kujifunza njia nyingine za kupata pesa mtandaoni endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

69 comments
 1. Kufanya biashara hii kwa sasa n almost 30,000 and nataka nijue kuwa 10 dollars nalipwa iwapo mtu atajiunga au iwapo mtu atatembelea link nayoipost mimi

 2. Na kwenye malipo imekataaa sijajua tatizo ni nini maana mi nshazoea kuitumia credit ? yangu kuinunulia vitu playstore au itakua nimekoseea wap. And kama itawezekana naomba niwaone kwa maelezo zaid. Coz am too interested in this busness aiseeee

   1. Kijuu kwa maelezo zaidi ingia katika tovuti hiyo baada ya kutafuta domain yako kisha click kwenye kitufe kilichoko kulia kilicho andikwa support hapo utapata maelezo yote na utaweza kuchat na wenyewe moja kwa moja. Pia unalipwa pale mtu atakapo nunua.

  1. Asante imani tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia fomu inayopatikana kwenye WASILIANA NASI hapo chini, tutakusaidia.

 3. ila sina ujuzi wowote kuhusu hii biashara maana nilipenda zaidi nianzishe website yangu mwenyewe,gharama ni kiasi gani kuanzisha website yangu? napatika mkoa wa Mbeya namba yangu 0758741531

 4. Comment*hichi kitu ni kweli au, maana kuna mitandao mingi kama hiii like paid2refers na mingine lakin ni yautapeli na kupotezeana mida..

  1. Ally unatakiwa kutumia link ambayo iko kwenye maelezo hapo juu, Kama una swali zaidi unaweza kuuliza kupitia kipengele cha majadiliano na tutaweza kukusaidia zaidi wewe na watu wengine wenye swali kama lako.

 5. hiyo link hapo juu ndio ninayoitumia
  web space starter 15GB 12months_ 51852.80
  kuna vitu vingine vingi mpaka inafika tsh 77916.37 lakini unalipa kwa dollar 34.08

 6. Kweli hii biashara inalipa au kuibiwa tu hela ya usajili na kutoona dollar 10 kila mteja anapoingia kwenye website?

 7. anhahaaa! Kweli wabongo tupo kutapeliwa kwa kupenda vitu vya mtelemko?ww na akili zako timamu unaanzaje kwanza!

 8. Hellow . Nime jaribu sana ila kutia account yangu ina kataa naomba msaada wenuu .. kwa mfano nataka kununua kitu au kuji rejister master card kwenye smart phone haikubali .. Help me guys

  1. Asanteeee kwa yako huduma na taarifa lakin kwa hili unaloliongelea inaonekana c kweli kwa sababu mm mpaka sasa nimefikisha $ 600 na nakuja namna yoyote ambayo hiyo hela inaweza kutoka …….VP unazungumziaje hili swala

 9. Japokua sijaelewa vizuri kwenye malipo hapo. Inamaana ulipwakwakumshirikisha mtu tuu au kunashughuli nyingine zitakazo fanya ulipwe

 10. Ahsante sana Kwa elimu nzuri, hakika Tanzania tunaweza.
  Kwani kutengeneza weɓsite au ɓlog ni ɓure au mpka pesa

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use