Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Infinix Mbioni Kuja na Simu Mpya ya Infinix Zero 6

Baada ya Infinix Hot 7 sasa ni toleo jipya la Inifnix Zero 6
Simu mpya ya Infinix Zero 6 Simu mpya ya Infinix Zero 6

Kampuni ya Infinix hivi karibuni imekuwa inajiandaa na ujio wa simu yake mpya ya Infinix Zero 6, Kama utakumbuka vizuri ni takribani miaka miwili toka kampuni ya Infinix ilipo zindua toleo la simu ya Infinix Zero 5, toleo ambalo ndio muendelezo wa simu hii mpya ya Infinix Zero 6.

Kwa mujibu wa tovuti ya techweez, simu hii mpya inategemewa kuzinduliwa nchini Kenya kati ya kuanzia siku ya leo tarehe 19 hadi mwanzoni mwa mwezi wa tatu. Kwa sasa bado tarehe ya kuzinduliwa kwa simu hiyo haijajulikana rasmi hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech kujua pale simu hii itakapo zinduliwa.

Advertisement

https://tanzaniatech.one/finder/specs/infinix-zero-6/

Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali, Infinix Zero 6 inasemekana kuja na kioo cha inch 6.2 chenye ukingo wa juu maarufu kama Top Notch, pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Kwa mbele simu hii inasemekana kuja na kamera ya Megapixel 16, huku ikisaidia na Flash ya LED Flash.

Kwa nyuma simu hii inasemekana kuja na kamera mbili, moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 13 huku zote zikisaidiawa na teknolojia ya HDR pamoja na Flash ya LED Flash.

Infinix Zero 6 Price in Tanzania

Mbali ya hayo, inasemekana kuwa Infinix Zero 6 itakuwa inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 660 MSM8956 yenye speed ya Octa core (2.2 GHz, Quad core, Kryo 260 + 1.8 GHz, Quad core, Kryo 260), yenye kusaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 64, hata hivyo ukubwa huo unaweza kuongezwa na memory card ya hadi GB 256.

Kwa upande wa mfumo wa undeshaji, inasemekana kuwa Infinix Zero 6 itakuja na mfumo wa Android 8.1, mfumo ambao unaweza kusasishwa hadi toleo jipya la Android 9.0 (Pie), Simu hii pia itakuwa inatumia mfumo mpya wa Infinix wa XOS Honeybee.

Kwa sasa inasemekana simu hii itauzwa kwa kati ya Shilingi za Kenya Ksh 25,000 hadi Ksh 26,500 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 582,000 hadi Tsh 620,000. Kumbuka bei hizi ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Infinix unaweza kusoma hapa kujua sifa za simu mpya nyngine ya Infinix Hot 7, na kama unataka kujua sifa kamili za simu hii mpya ya Infinix Zero 5, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use